Home Kitaifa MAKAMU RAIS DKT. PHILIP MPANGO ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA 19

MAKAMU RAIS DKT. PHILIP MPANGO ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA 19

Makamu wa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango ameshuhudia utiaji saini wa mikataba mbalimbali wakati akifunga Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya mwaka 2022.

Mikataba hiyo 19 iliyotiwa saini Julai 13, 2022 imejumuisha mikataba tisa ya uwekezaji kwenye kongani ya viwanda ya sino Tan yenye viwanda 200 vyenye thamani ya dola bilioni 3 na inatarajiwa kutoa ajili za moja kwa moja zaidi ya laki moja.

Mikataba mingine imejumuisha sekta za kilimo, ufugaji na utebgenezaji wa mitambo na mashine mbalimbali ikiwa ni matokeo ya kongamano la wawekezaji, wanunuzi na wauzaji lililofanyika Julai 5, 2022 ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Kibiashara 2022.

Akiongoza zoezi la utiaji saini mikataba hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara. Prof. Godius Kahyarara amesema kongani hiyo ni ya kwanza kwa ukubwa kwa nchi za kusini mwa Afrika ambapo pia zoezi la utoaji wa motisha kwa kampuni tatu zilizosajiri miradi yake kupitia kituo cha uwekezaji nchini TIC limefanyika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!