Home Kitaifa LUSHOTO YAPATA KITUO KIPYA CHA POLISI BAADA YA MIAKA 193.

LUSHOTO YAPATA KITUO KIPYA CHA POLISI BAADA YA MIAKA 193.

Na Boniface Gideon, LUSHOTO

KITUO Cha Polisi Cha Kwanza kujengwa Nchini Tanzania Kilikuwa Wilayani Lushoto Mkoani Tanga ilikuwa ni mwaka 1829 na mpaka Leo hii Bado kipo vizuri huku kwakipindiki chote hicho Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga lilikuwa likikitumia .

Historia ilibadilishwa mwishoni mwa Wiki hii Baada ya Kuzinduliwa Kituo kipya nakuvunja mwiko , Mwishoni mwa Wiki hii Kulikuwa na Sherehe kubwa hususani kwa Maaskari Wilayani humo pale Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi akiongozwa na mkuu wa Mkoa wa Tanga Omar Mgumba kuzindua Kituo hicho chenye VIP ya Mahabusu.

Akizungumzia Kituo hicho mkuu wa Mkoa wa Tanga Omar Mgumba Alisema historia imeandikwa kwa Ujenzi huo ,
Kwenye maisha yangu yote sikuwahi kufikiria kuwa Kuna VIP ya Mahabusu ndio nimeona Leo hii Tena ipo kwa Wanawake na Wanaume , tunamshukuru Sana Rais Samia kwakutuletea Fedha zilizofanikisha Ujenzi huu ” Alisisitiza

Aliwataka Askari kufanya kazi kwa bidii na kutenda Haki ,
Askari wetu fanyeni kazi kwa bidii lakini pia mtende Haki , kuhusu suala la kutaka eneo kubwa zaidi kwaajili ya mazoezi tutakwenda kujadiliana na Wenzetu wa Halmashauri kuona namna yakuwapatia eneo ambalo lipo wazi Mana maeneo mengi ya Halmashauri yapo kibiashara kwaajili ya kuingiza mapato” Alisisitiza Mgumba

Kwaupande wake Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Hamad Masauni Alisema Serikali inaendelea kuboresha huduma za kijamii ,

Serikali inaendelea kuboresha huduma za kijamii ikiwamo Ujenzi wa vituo vya Polisi vya kisasa na tutaendelea kujenga vingine mpaka lengo la Serikali litimie” Alisisitiza Masauni

Aidha alimpongeza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Safia Jongo na Wasaidizi wake kwakufanikisha kujengwa kwa Kituo hicho kwa viwango vya Hali ya juu,
Nikupongeze Wewe RPC pamoja na Wasaidizi wako kwakusimamia vyema Ujenzi wa Kituo hili kwa Viwango vya Hali ya juu , tutaendelea Kuleta Fedha zaidi kwaajili ya kufanikisha Ujenzi wa vituo vingine pamoja na kuboresha Mazingira kwa Askari wetu” Alisisitiza Masauni

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!