Home Kitaifa LEAT NA RUSUDEO WATOA HATI ZA HAKI MILIKI ZA KIMILA 4,530 NKASI

LEAT NA RUSUDEO WATOA HATI ZA HAKI MILIKI ZA KIMILA 4,530 NKASI

Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Rukwa Bw. Swagile Msananga (Kushoto) akikabidhi sehemu ya Hati za Haki Miliki za Kimila kwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Queen Sendiga (kulia) leo ili azikabidhi kwa wananchi wa kijiji cha Tambaruka wilaya ya Nkasi.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Peter Lijualikali (katikati) akimtambulisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Queen Sendiga kwa viongozi leo alipowasili kijiji cha Tambaruka kuzindua zoezi la ugawaji Hati za Haki Miliki za Kimila zilizotolewa na mashirika ya LEAT na RUSUDEO kwenye vijiji vitatu vya Nkasi.
Mkurugenzi wa Kukuza Uchumi USAID Tanzania Bw. Colin Dreizin akizungumza kwenye halfa ya ugawaji Hati za Haki Miliki za Kimila kwa wananchi wa kijiji cha Tambaruka wilaya ya Nkasi leo ambapo taasisi za LEAT na RUSUDEO zinatekeleza mradi huo kupitia ufadhili wa watu wa Marekani.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wa Rukwa Mhe. Queen Sendiga (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa zoezi la utoaji Hati ya Haki Miliki za Kimila 4,530 kwa vijiji vya Tambaruka, Lyele na Kisula wilaya ya Nkasi ziliztolewa na taasisi za LEAT na RUSUDEO .

Na. OMM Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga amepongeza Timu ya Wanasheria Watetezi wa  Mazingira kwa Vitendo  (LEAT) na Shirika la Maendeleo Endelevu Rukwa ( RUSUDEO) kwa kufanikisha utoaji wa Hati Za Haki Miliki za Kimila 4,530 kwa wananchi wa vijiji vitatu vya Tambaruka, Lyele na Kisula wilaya ya Nkasi.

Pongezi hizo amezitoa leo (Oktoba 26,2022) wakati akizindua zoezi la ugawaji hati hizo kwenye kijiji cha Tambaruka ambapo amesema zinakwenda kuwa msaada kwa wananchi kiuchumi pamoja na kusaidia kuondosha migogoro ya ardhi.

Naomba viongozi wa ngazi zote kuanzia wenyeviti wa vitongoji, vijiji na madiwani shirikianeni na LEAT ili kutoa elimu  kuhusu faida za hati za haki miliki za kimila ili zoezi lisipotoshwe na watu wasiotakia mema wananchi. LEAT hawajaja kupoka ardhi yenu bali wamekuja kupima na kuwapa hati miliki za kimila na ardhi ni umiliki wenu” alisema Sendiga.

Kwa upande Msimamizi wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Maliasili Bi. Hana Lupembe alisema mradi huo wa miaka mitano ulianza mwaka 2020 hadi 2025 umenufaisha vijiji 18 katika wilaya za Nkasi na Sumbawanga.

Mratibu huyo alitaja mafanikio mengine ni pamoja na kuwezesha halmashauri utengaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa vijiji 13 kati ya 18 sawa na asilimia 86 ya lengo na pia wametoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa wananchi 2,170 kati ya lengo la kuwafikia watu 1,798.

Mradi huo wa Usimamizi Endelevu wa Maliasili unatekelezwa na LEAT pamoja na RUSUDEO kwa ufadhili wa shirika la misaada la Marekani ( USAID) ambapo katika uzinduzi wa leo umehudhuriwa na Bw. Colin Dreizin ambaye ni Mkurugenzi wa Kukuza Uchumi USAID Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!