Home Kitaifa TMA YASHAURI SEKTA ZA SERIKALI NA BINAFSI KUFUATILIA UTABIRI KATIKA SHUGHULI MBALI...

TMA YASHAURI SEKTA ZA SERIKALI NA BINAFSI KUFUATILIA UTABIRI KATIKA SHUGHULI MBALI MBALI.

Na Hadia Khamis.
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini(TMA) imesema mikoa 14 inayopata msimu mmoja wa mvua inatarajiwa kunyesha mvua za chini ya wastani hadi wastani.

Akizungumza wakati akitoa utabiri wa msimu wa mvua Mkurugenzi wa huduma za Utabiri wa TMA,DK Hamza Kabwela wakati akitoa utabiri wa mwelekeo wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka unaoanzia Novemba 2022 hadi Aprili 2023, amesema mikoa inayotarajiwa kupata mvua hizo ni Kigoma,Tabora,Katavi,Singida,Dodoma,Ruvuma na Lindi.

Dk Kabwela aliitaja mikoa mingine ni Lindi,Mtwara,Njombe,Rukwa,Singwe,Mbeya,Iringa na kusinibmwa Morogoro

Amesema kunyesha kwa mvua hizo chini ya wastani imesababishwa na La Nina ambapo kutakuwa na joto la bahari la chini ya wastani katika eneo la kati la bahari ya Pasifiki linatarajiwa kuendelea kuwa chini ya wastani

DK Kabwela amesema Katika nusu ya kwanza ya msimu kuanzia Novemba mwaka 2022 hadi Januari mwaka 2023 vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza.

Ongezeko la mvua linatarajiwa katika nusu ya pili ya msimu kuanzia Februari hadi Aprili mwaka 2023 na mvua za nje ya msimu zinatarajiwa kunyesha Mei mwaka 2023 katika maeneo mengi,”amesema DK Kabwela.

Dk Kabwela amesema athari zinazotarajiwa kujitokeza upungufu mkubwa wa unyevunyevu katika udongo katika maeneo hayo yanayopata mvua hizo na kuathiri ukuaji wa mazao na upatikanaji wa malisho kwa ajili ya mifugo

Amesema athari zingine zinazotarajiwa kujitokeza kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kupungua na kuathiri upatikanaji wa maji kwa matumizi mbalimbali kama vike umwagiliaji na uzalishaji wa nishati.

Dk Kabwela amezisahuri mamlaka kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa pamoja na kuweka miundombinu ya uvunaji maji na kuandaa na kutekeleza mipango mkakati ya kuhimiza kilimo himilivu.

Hali hii inaweza kuathiri uoteshaji na ukuaji wa mazao hususan katika kipindi cha Novemba na Desemba 2022 kutakuwa na ongezeko la bisumbufu vya mazao kama vile mchwa,viwavijeshi ,panya vinatarajiwa kujitokeza katika msimu na kuarhiri mazao ya uzalishaji kwa ujumla pamoja na matukio ya moto yanaweza kujitokeza kutokana na vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa,“amesema Dk Kabwela.

Amesema wakulima wanatakiwa kupanda mazao na mbegu zinazokomaa kwa muda mfupi na zinazostahimi upungufu wa mvua kama vile mihogo,viazi mikunde na mazaobya bustani.

Pia katika upatikanaji wa maji na malisho kwa ajili ya mifugo na kupelekea uwezekano wa migogoro kujitokeza baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.

Naye Mtabiri wa Halii ya hewa(TMA) Joyce Makwata amesema matukio ya vipindi vya mvua kubwa yanaweza kujitokeza hata katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua chini ya wastani.

Upi uwezekano wa kutokea kwa migandamizo midogo ya hewa kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi ikiwa ni pamoja na rasi ya Msumbiji hivyo kusababisha vipindi vya mvua katika nusu ya pili ya msimu,”amesema Makwata.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!