Home Kitaifa NAIBU WAZIRI WA FEDHA AZINDUA PROGRAMU YA PhD CHUO CHA USIMAMIZI WA...

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AZINDUA PROGRAMU YA PhD CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM).

Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Kavuu, Mheshimiwa Laurent Luswetula (Mb), amezindua rasmi programu ya Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya KingJada, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mheshimiwa Luswetula alisisitiza umuhimu wa elimu ya juu katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi. Alieleza kuwa programu hiyo itachangia kuzalisha wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu, kuimarisha uwezo wa kufanya tafiti na ubunifu, pamoja na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali za kitaifa.

Aidha, alibainisha kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za taasisi za elimu ya juu katika kuimarisha rasilimali watu, ili kufikia malengo ya maendeleo ya taifa, ikiwemo Dira ya Maendeleo 2050.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha IFM, Profesa Emmanuel Mjema, alisema kuwa chuo hicho kinaendelea kujizatiti kufikia malengo yake ya kitaasisi, akisisitiza umuhimu wa elimu ya juu hususan katika taaluma za fedha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!