Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, ametia saini kitabu cha wageni katika Ofisi za CCM Mkoa wa Geita na kuzungumza na viongozi wa Chama wa mkoa huo.
Kinana akizungumza na viongozi hao, amewataka kuendeleza ushirikiano uliopo ambao amesema ni nyenzo muhimu na msingi sahihi kwa maendeleo ya jamii.
Pia, amepongeza kazi kubwa inayofanywa na viongozi wa Chama na serikali mkoani humo huku akiwasisitiza viongozi na watendaji kuendelea kutatua changamoto za wananchi ili kuharakisha maendeleo.