Home Kitaifa KIKAO CHA USHIRIKIANO BAINA YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA OFISI YA...

KIKAO CHA USHIRIKIANO BAINA YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA OFISI YA RAIS (SMZ) CHAFANYIKA JIJINI DODOMA

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu imepata ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar ambao umelenga katika kubadilishana uzoefu katika masuala ya kazi, maendeleo vijana, ukuzaji ajira na ustawi wa Watu wenye Ulemavu.

Mkurugenzi Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Bw. Rashid Maftah (kulia) akiwasilisha taarifa kuhusu shughuli zinazotekelezwa na kitengo hicho wakati wa kikao cha Ushirikiano baina ya ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar kilichofanyika Oktoba 13, 2022, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Dkt. Islam Salum akizungumza wakati wa kikao cha Ushauriano baina ya ofisi hiyo na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Oktoba 13, 2022 Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma. Kikao hicho kililenga kujadili utekelezaji wa shughuli zinazotekelezwa na ofisi hizo kwa pande zote mbili.

Ugeni huo umeongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais anayesimamia masuala ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji. Katika kikao hicho ofisi hizo zimedhamiria kushirikiana kwa karibu katika kutekeleza majukumu sambamba na kutoa huduma kwa wananchi kwa tija na ufanisi katika pande zote mbili za Muungano.

Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Dkt. Islam Salum wakati wa kikao cha Ushauriano baina ya ofisi hiyo na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Oktoba 13, 2022 Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.

Aidha, katika kikao kazi hicho Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Kazi, Uchumi na Uwekezaji aliambatana na Kamishna wa Kazi – Zanzibar pamoja na Mkurugenzi wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSH) – Zanzibar.

MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!