Home Kitaifa KAMANDA MUTAFUNGWA; ATOA MAAGIZO KWA WAMILIKI WA MAGARI YANAYOBEBA WANAFUNZI

KAMANDA MUTAFUNGWA; ATOA MAAGIZO KWA WAMILIKI WA MAGARI YANAYOBEBA WANAFUNZI

Na Magrethy Katengu

Jeshi la polisi Kikosi cha Usalama barabarani kimewataka wamiliki wa magari yote yanayobeba wanafunzi kuhakikisha wanayafanyia ukarabati wa mara kwa mara ili kusaidia kudhibiti ajali zinatokea na kusababisha vifo vya watu na wengine kupoteza maisha.

Agizo hilo limetolewa Dar es salaam na Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchi Wilbroad Mutafungwa katika zoezi la Ukaguzi wa magari yanayobeba wanafunzi kwenda shuleni iliyojumuisha Wilaya tano za Mkoa huo huku zoezi likiendelea kufanyika Nchi nzima ambapo amesema katika ukaguzi huo uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam magari yapatayo 100 yalijitokeza kukaguliwa huku yakimainika na mapungufu ikiwemo uchakavu wa bodi,Mfumo wa breki, matairi,mpangilio wa viti pamoja na mikanda yakujiunga wanafunzi wakiwa katika safari ya kuenda na kurudi shuleni.

“Kuna Mambo mnakuwa mnazembea mkiona ni madogomadogo lakini yamekuwa na athari kubwa sana hasa ajali ikitokea katika magari mengi nimekagua siti hazina ubora zimelegea mikanda hakuna hivyo ikitokea gari limepata msukosuko ikiwemo breki kufeli inapelekea mwanafunzi kurushwa dirishani au kiti kugeuka kumdondokea hivyo yuko hatarini kuumia niwatake katika hili hakikisheni siti zinafungwa vizuri hatutapasisha gari lolote likiwa na mapungufu”amesema Mutafungwa

Kamanda Mutafungwa amesema zoezi hilo lilianza kufanyika nchi nzima kuanzia June 3 hadi Julai mwaka huu na ya magari elfumbili na tisini katika zoezi hilo tukikuta magari yaliyokuwa na Matatizo makubwa yalilazimika kuondolewa namba za usajili ili yakafanyiwe marekebisho tena miamoja thelathini na saba ambayo hayakuwa na ubovu wowote yalikuwa elfumoja miatano na tisini na nne na yaliyokuwa na Matatizo ni miatatu hamsini na tisa nchi nzima.

“Ukaguzi huu tunaufanya ni kutokana na mahitaji ya kisheria ambayo inataka magari yanayobeba wanafunzi haya yakaguliwe mara mbili kwa mwaka mwishoni mwa mwezi wa 6 na mwishoni mwa mwezi wa 12 Jeshi la Polisi kikosi Cha Usalama Barabarani tuongeze nguvu zaidi kuyakagua magari ya Wanafunzi katika mikoa yote nchini”amesema Mutafungwa

Hata hivyo amesema wanaendelea na ukaguzi huo katika kipindi hiki ambapo shule zimefungwa ili kuhakikisha ifikapo Septemba 5 ambapo shule zote zinapofunguliwa magari yote ambayo yamekutwa na kasoro wamiliki wawe wameyafanyia ukarabati au kuyaondoa Barabarani.

“Niwatake wakuu wa usalama Barabarani, wa madawati ya elimu ,ya ukaguzi wa magari nchi nzima magari hayo yakaguliwe mifumo yote ikiwemo ubora wa bodi,viti,matairi,usukani,breki ili shule zinapofunguliwa yanakuwa na ubora wa kuweza kutembea Barabarani huku yakiwa yamebeba wanafunzi”amesema Kamanda

Hata hivyo amesisitiza kwa wale Wamiliki wa magari na wadereva watakaokaidi tutatoa namba za usajili,hivyo niwaombe wazazi wa wanafunzi wa shule,Wasimamizi wa Watoto,wakuu wa shule pamoja na Madereva kushirikiana na Jeshi la Usalama Barabarani katika kuzuia hizi ajali Barabarani.

Katika ukaguzi huo amewasisitiza Madereva ambao hawana leseni daraja “C”kutoka chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji( NIT) na Chuo Cha Elimu ya Mafunzo ( VETA) hawaruhusiwi kuendesha magari ya Wanafunzi hivyo katika kipindi hiki wanafunzi wakiwa likizo Madereva ambao hawana leseni hizo wanapaswa kujiendeleza kitaaluma ili wapate leseni ya daraja

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!