Home Kitaifa IBRAHIM NDORO ACHAGULIWA KUWA MWEYEKITI WA CCM WILAYA YA RUANGWA

IBRAHIM NDORO ACHAGULIWA KUWA MWEYEKITI WA CCM WILAYA YA RUANGWA

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wilayani Ruangwa kutoka kata 22 wamemchagua Ndugu Ibrahim Issa Ndoro kuwa Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo.

Katika Mkutano huo ambao uliofanyika Oktoba 2, 2022 pia ulihuduriwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Ndugu Ndaro aliibuka mshindi katika Mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Awali na Msingi, Wonder Kids.

Ndoro alijizolea kura 921 na kuwabwaga washindani wake, Rashid Nakumbya aliyepata kura 21 na Fatuma  Rashidi Ng’ombo aliyepata kura 17. Jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 966, kura 7 ziliharibika .

Aidha katika uchaguzi huo, Msimamizi wa uchaguzi Shaibu Ndemanga aliwatangaza Ndugu Ramadhani Ibrahim Matola aliyepata kura 663, Julius Charles Mukheben aliyepata kura 640 na Hassan Twaha Ngoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa aliyepata kura 557 kuwa washindi wa nafasi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa.

Pia Ndugu Kasambe Hokororo alichaguliwa kuwa Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!