Home Kitaifa HAJI MANARA AMWAGA MAMILIONI , VIFAA VYA NYUMBANI NA ZAWADI KIBAO ,...

HAJI MANARA AMWAGA MAMILIONI , VIFAA VYA NYUMBANI NA ZAWADI KIBAO , MAGIFTI DABO DABO DROO YA PILI

PICHA YA PAMOJA : Mshindi wa Vifaa vya Nyumbani kutoka Hisense ambavyo ni FRIJI , MICRO WAVE , TV , na SOUNDBAR  Kampeni ya MAGIFTI DABO DABO Droo ya PILI Bwn. Abdul Said katika picha ya pamoja na HAJI MANARA Semaji la Magifti Dabo Dabo , kulia ni Mkewe ambaye amemchagua kushinda nae ambaye na yeye atapewa vifaa hivyohivyo kutoka HISENSE .

Bw. Eginga  Mohammed – Meneja wa Bidhaa za Intaneti Tigo ( kushoto ) na Haji Manara Semaji la Kampeni ya Magift Dabo Dabo ( kulia ) wakikabidhi Hundi ya Shilingi Milioni moja kwa baadhi ya washindi wa Pesa Taslim Kampeni ya Magifti Dabo Dabo Droo ya Pili , Mapema leo hii Makao makuu ya Tigo PSSSF Commercial Complex Jijini Dar Es Salaam.

Na Mwandishi Wetu. 

DROO ya Pili ya kampeni ya ‘Magifti Dabodabo’ imefanyika ambapo washindi 13 wamepatikana kutoka mikoa mbalimbali nchini na kupatiwa zawadi zao , Washindi hao ni washindi wa Milioni 5 , Milioni moja , safari za DUBAI NA ZANZIBAR pamoja na Vifaa vya nyumbani kutoka HISENSE

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo jijini Dar es Salaam , Bw. Eginga  Mohammed – Meneja wa Bidhaa za Intaneti Tigo amesema katika droo ya pili wamewapata washindi mbalimbali wakiwemo wa safari ya Dubai, Zanzibar, vifaa vya ndani na fedha taslimu.

Alisema washindi wa kampeni ya Magifti Dabodabo’ msimu huu wa mwisho wa mwaka wanapata fursa ya kuchagua wenza wao au watu wa karibu kwa ajili kuwapendekeza kupata zawadi.

“Tumefanya droo ya pili na kupata washindi wa zawadi mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, kampeni ya Magifti Dabodabo inatoa fursa kwa washindi kuchagua wenza wao au watu wa karibu kujidhindia zawadi kama zao,” alisema.

Msemaji wa Kampeni ya Magifti Dabodabo, Haji Manara alisema Tigo imezindua kampeni hiyo kwa ajili ya kurejesha wanachokipata kwa jamii.

Alisema washindi walipatikana kutokana na kufanya miamala mbalimbali ikiwemo ya Tigo Pesa, kununua salio la muda wa maongezi na umeme wa luku.

Aliwataka wateja wa Tigo kuendelea kutumia mtandao huo kufanya miamala mbalimbali kuhakikisha wanaingia katika droo zingine kwani kampeni itaendeshwa kwa muda wa siku 80 nchi nzima.

“Tunawaomba wateja kuendelea kufanya miamala mbalimbali ili kuingia katika droo ya Magifti Dabodabo, kampeni itaendeshwa kwa muda wa siku 80 na kuna zawadi kubwa ya magari mawili mapya,” alisema Haji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!