Na Mwandishi Wetu
Wakala wa Barabara Za Vijijini na Mijini (Tarura) Umesema kuwa bado Kuna uelewa mdogo wa Wananchi na Baadhi ya Viongozi juu ya Ujenzi wa Madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe na Tofali za kuchoma.
Hayo yamebainishwa Leo Jijini Dodoma Na Injinia Victor Seif Mtendaji Mkuu wa Tarura, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari juu ya ubora na uimara wa teknolojia mpya ya Ujenzi wa Madaraja kwa kutumia Mawe na Tofali.
Injinia Seif Amesema Tarura imeanza Ujenzi wa Madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe na Tofali lakini bado kumekuwa na uelewa mdogo kwa Baadhi ya Wananchi na viongozi wa kisiasa katika Maeneo ya mradi.
“Sisi Kama Tarura tumeweza kuja na Teknolojia hii ambayo imekuwa ikipunguza gharama kubwa za Ujenzi kwq zaidi ya asilimia 50% kuliko ukitimia mondo na saruji” Amesema Injinia Seif.
Ametaja kuwa katika Mkoa wa Kilimanjaro walitenga zaidi ya Milioni 400 kwa ajili ya Ujenzi wa Daraja moja kwa kutumia nondo na saruji lakini walivyoamua kutumia teknolojia ya mawe fedha hiyo imeweza Kujenga Madaraja Matatu zaidi.
Amesema kuwa Ujenzi huo ni rahisi kwakuwa unafanyika katika Maeneo ambayo Kuna mawe hivyo serikali inakuwa gharama yake ni saruji na utaalamu kutoka Kwa Waandisi wa Tarura.
Ametaja kuwa Kuna Baadhi ya maeno wamekuwa wakiwatumia hata Mafundi wa kawaida na kuwafundisha namna ya Kujenga barabara na Madaraja kwa kutumia Mawe.
Injinia Seif ametaja kuwa mpaka Sasa ni zaidi km 20 za barabara zimejengwa kwa mawe mkoani Mwanza huku km Zaidi ya 40 zikiwa zimejengwa mkoani Kigoma.
Kwa upande wake Mhandisi Mtaalamu wa Ujenzi wa Madaraja kwa kutumia Mawe Mhandisi Pharesi Ngeleja ametoa wito kwa Tasisi mbalbali za Ujenzi kujitokeza kwa wingi kujifunza teknolojia hiyo kutoka Tarura.
Amesema Tasisi Kama TANROADS na zingine zikiweza kutumia mfumo huo utaokoa gharama za Ujenzi kwa zaidi ya asilimia 50% na kutaja kuwa Madaraja ya Mawe yameonyesha kuwa yanaishi muda mrefu kuliko ya nondo na saruji.
Ametaja kuwa Madaraja yote yaliyopo katika Reli ya kati yalijengwa kwa teknolojia hiyo na mpaka leo bado yanatumika na hayajaonyesha kuchoka.