Home Kitaifa MBARAWA AITAKA DIT KUPUNGUZA GHARAMA MFUMO WA GESI KWA MAGARI

MBARAWA AITAKA DIT KUPUNGUZA GHARAMA MFUMO WA GESI KWA MAGARI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa ameitaka Tasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Kuangalia namna itakavyo leta unafuu katika mradi wa ufungaji mfumo wa gesi kwa magari hapa Nchini.

Waziri Mbarawa Amesema hayo Mapema Leo Jiji Dodoma wakati alipotembelea Maonyesho katika Mkutano wa 19 Bodi ya Usajili wa Wahandisi Nchini uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention center.

Hii ni teknolojia nzuri na itatusaidia sana kupambanana hizi changamoto lakini tuangalie namna ya kuweza kupunguza gharama za ufungaji.” Amesema Waziri Mbarawa.

Amesema kuwa ukiachilia mbali kupunguza Bei Tasisi hiyo inapaswa kufanya mchakato wa haraka kuyafikia magari yanayotumia Disel hili nayo yaweze kufaidika na gesi asilia.

Waziri Mbarawa amefungua milango kwa DIT kufika kumuona kwa ushauri kwani licha ya yeye kuwa Waziri lakini amechapisha maandiko manne yauyuso teknolojia ya gesi asilia katika matumizi ya magari.

Kwa upande wake Mhadhiri kutoka DIT, Dk. John Msumba alimuhakikishia Waziri kuwa Tasisi yake inqfanya kila namna ufungaji huo wa gesi uwe kwa Bei nafuu lakini changamoto kubwa wanayokutana nayo ni Kodi ya vipuri wanavyoingiza kutoka nje.

DIT inatamani kufunga vifaa hivyo Bei nafuu kwa utumiaji wa gesi ni Rafiki wa mazingira lakini changamoto kubwa ni wanapoingiza vifaa hivyo Bandarini kwani mpaka Sasa avijapatiwa msamaha wa Kodi” Amesema Dk. Msumba.

Alimaliza kwa kuishukuru serikali na Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Samia Suluhi Hassan kwa kuendelea kuishika mkono Tasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!