Home Kitaifa DKT. KIJAJI ATOA WITO KWA WATANZANIA KUTOA MAONI MABORESHO YA SHERIA MPYA...

DKT. KIJAJI ATOA WITO KWA WATANZANIA KUTOA MAONI MABORESHO YA SHERIA MPYA YA UWEKEZAJI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ametoa wito kwa watanzania kutoa maoni kuhusu maboresho ya Sheria mpya ya Uwekezaji.

Ameyasema hayo leo Septemba 30, 2022 jijini Dar es Salaam katika uzinduzi rasmi wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji linalounganisha wafanyabiashara wa Tanzania na Italia.

Kwa mujibu wa Dkt Kijaji hadi sasa uwekezaji wenye thamani ya Dola bilioni mbili za kimarekani umeshafanyika hapa nchini kutoka kampuni za Italia.

Ameongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kwa dhati kuwalea vema wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kwa kupunguza kiasi cha fedha anachotakiwa mwekezaji kuwa nacho ili aweze kujisaliji katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)

Naye Balozi wa Tazania nchini Italia Bw. Mahmoud Kombo amewahimiza watanzania kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali kama vile fursa zinazopatikana katika sekta ya utalii kupitia filamu ya The Royal Tour. Pia amewahimiza watanzania kujitokeza kwa wingi kufanya biashara na kampuni za nje hasa za kutoka Italia

Kwa Upande wake Balozi wa Italia nchini Tanzania Marco Lumbardi amesema hadi sasa miradi yenye thamani ya Dola Bilioni mbili za kimarekani imewekezwa hapa nchini na kampuni kutoka Italia.

Aidha, Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture, (TCCIA) Bw. Paul Koyi amesema jukwa hilo limesaidia kupatikana kwa makubaliano ya pamoja na Chemba ya Genova ya Italia ambayo yanatarajiwa kuleta mafanikio na faida baina ya Nchi hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here