Home Kitaifa DC GONGWE: WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU WATHAMINIWE

DC GONGWE: WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU WATHAMINIWE

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe ameitaka jamii kuwathamini watoto wenye mahitaji Maalumu Kwa kuwapatia haki zao za msingi kiwemo Elimu,Afya na kwani nao Wanaweza kwama watoto wengine.

DC Gondwe ametoa rai hiyo wakati wa Tamasha la Watoto wenye Mahitaji Maalumu lililoandaliwa na Kijiji Cha Makumbusho ya Taifa lenye ujumbe usemao”Haki Sawa kwa Wote” lengo ni kuwakutanisha Watoto wenye Ulemavu wa aina mabalimbali ikiwemo ulemavu wa viungo na walemavu wa ngozi( Albino) na wasioo wasiona,walemavu wa viungi na Viziwi .

Hata hivyo amesema kwamba Watoto wenye ulemavu wanatakiwa,kutambuliwa, kuthaminiwa na kupatiwa haki zao za msingi ikiwemo elimu ili kuwafanya waweze kuishi katika maisha bora ,huku akikemea jamii kuacha vitendo vya unyanyapaa,kuwaficha watoto hao.

“Mimi nakemea ukatili kwa watoto wenye mahitaji hapana hivyo wito kwa wazazi wakae karibu na watoto wao na sio wawaachie wafanyakazi wa Nyumbani kwani wengi wao wamekuwa wakibainika kuwawafanyia ukatili watoto na kutokomea kuwa watoto wa mtaani na kuwa ombaoba ’amesema DC Gondwe

Hata hivyo amekipongeza Kijiji cha Makumbusho ya Taifa kwa kuandaa tamasha hili ambalo limelenga kutambua thamani ya Watoto wenye ulemavu,natoa wito kwa jamii,taasisi na mashirika mbalimbali kuendelea kuwathamini watu wenye ulemavu

Watoto wenye ulemavu kutoka shule mbalimbali za msingi ikiwemo shule ya Mgabe,Shule ya Msingi mchanganyiko,Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu ,wamekutana kwenye tamasha hilo nakuweza kushiriki Mambo mbalimbali ikiwemo michezo na burudani.

Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Kijiji Cha Makumbusho Bi.Wilhelmina Joseph amesema kwamba Makumbusho ya Taifa itaendelea kuthamini makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo Watoto wenye mahitaji mbalimbali ili kuwafanya wapate haki zao za msingi.

“Tumeandaa tamasha hili ili kuthamini haki za Watoto hawa ,hivyo sisi Kama Makumbusho ya Taifa tumeandaa tamasha hili la Watoto wenye mahitaji Maalumu na tukaweka kauli mbiu ya Haki Sawa kwa Wote” ili kuifanya jamii itambue kuwa hata watu wenye ulemavu wana haki sawa na wengine hivyo wasiwafiche majumbani” amesema Bi Wilhelmina.

Akizungumza kwa niaba ya Walimu Wenzake kutoka shule hizo Bw.Emanuel Ibrahim kutoka shule ya Msingi ya Jeshi la Wokovu ( Salvation Army) amesema kwamba ulemavu siyo kushindwa hivyo wameiomba Makumbusho ya Taifa kulifanya tamasha hilo kuwa endelevu.

Naye Mwanafunzi kutoka Shule ya Jeshi la Wokovu Theresa Fredric ameshukuru kwa Upendo waliooneshwa kukutanishwa kwa pamoja na Shule nyingine kuonesha vipaji vyao ikiwemo uimbaji,kutangaza kama Waandishi wa habari kwani na wao Wanaweza

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!