Na Magrethy Katengu
.
Uwekezaji wa huduma za kifedha wazidi kuongezeka nchini Tanzania kwani leo Benki ya China Dasheng imefungua tawi lake jipya la pili Kariakoo Jijini Dar es salaam Mtaa wa Lumumba ili kusaidia kuwarahisishia Wafanyabiashara kwa kusogeza huduma karibu na wateja wao wengi wenye kutumia benki hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki CHENG JI amesema benki hiyo tangu kuanzishwa kwakwe Ina miaka minne hivyo wameamua kuja kuanzisha hapa Tanzania ni kutokana Tanzania kuwa na mashirikiano ya kibiashara kuagiza bidhaa nyingi kutoka nchini China hivyo itasaidia kufanya huduma zao za kifedha kulipia bidhaa zao kwa urahisi .
“Benki hii iko vizuri haina ubaguzi wowote kwani walioajiriwa Watanzania nao wamepata fursa ya ajira hivyo pia tunatarajia kwenda nchini China kuanzisha tawi lingine la kutoa huduma hii ya kifedha kwa Wafanyabiashara kutoka Tanzania na China kutumia benki hii” amesema Cheng J
Hata hivyo amesema kuwa benki hiyo itatoa huduma Kwa wafanyabiashara Wakubwa, wadogo, na kati kwani itakuwa ni chachu ya kukuza uchumi baina ya nchi ya Tanzania na China kupitia wafanyabiashara wote hao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa bodi ya Benki ya China Dasheng Poniwoa Mbisse ameishukuru benki hiyo kwa kufungua tawi lake karibu na wafanyabiashara wa kariakoo likiwa ni tawi la kwanza la benki ya China na litasaidia kuwaunganisha wafanyabiashara wa Kitanzania na China na kurahisisha biashara baina ya Tanzani na China.
Aidha amewaomba watanzania kutumia benki hiyo yenye viashiria vya China kuitumia benki hiyo katika kufanya biashara zao kwani ni benki ambayo ndani ya miaka minne tu Tanzania,tayari imeonyesha mwanga wa mafanikio katika uwekezaji.