

Na Boniface Gideon, TANGA
Zaidi ya Wasichana 900 ambao hawakufanikiwa kupata Elimu katika mfumo maalumu wa Elimu ya upili ( Sekondari) wamefanikiwa kupata Elimu hiyo kupitia Mradi wa Elimu na Stadi za Maisha unaotekerezwa na Shirika la BRAC MAENDELEO TANZANIA katika Mkoa wa Tanga.
Meneja wa Mradi huo Hope Jasson aliwaeleza Jana Wadau wa Maendeleo Jiji la Tanga Wakati wa Kikao Cha kujadili na kutathmini mafanikio ya Mradi huo pamoja na namna ya kuendeleza Miradi inayoachwa na Shirika Hilo kutokana na Mradi huo wa Miaka kuishia ukingoni Desemba 30 mwaka huu.
Hope Alisema BRAC MAENDELEO TANZANIA Chini ya Ufadhili wa Shirika la Norad la Nchini wamefanikiwa kuwapatia Elimu ya Sekondari Mabinti hao zaidi ya 900 chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,

” Asilimia 86.8 ya Wasichana walioko kwenye Rika Balehe wamefaulu na kupewa Cheti Cha Elimu ya Sekondari kuanzia Mwaka 2017 Hadi 2021,
Vituo 30 vya Masomo vinaendelea ya Elimu chini ya usimamizi wa Jamii ambapo Kati ya hivyo Vituo 20 vipo katika Halmashauri ya Jiji la Tanga na 10 vipo Wilaya ya Korogwe ” Alisisitiza Hope
Alisema Wasichana zaidi ya 1161 walipatiwa Mafunzo ya kuanzisha Biashara ndogo pamoja na Mitaji kupitia SIDO,VETA na Ustawi wa Jamii,
“Zaidi ya asilimia 65 ya Wasichana hususani katika Halmashauri ya Jiji la Tanga Wanajishughulisha na shughuli za kujiongezea kipato na kubadili mfumo wao wa Maisha ya awali kabla ya kupata Elimu ” Alisisitiza Hope
Aliongeza kuwa Wasichana 10 wa wamefanikiwa kujiunga na Chuo kikuu kwa kozi za Shahada ya Kwanza huku Wasichana 22 Walioko kwenye Rika Balehe Wamehitimu ngazi ya Cheti kutoka Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Kampasi ya Tanga Wakati,
“Wasichana wengine 3 waliandikishwa katika Vyuo mbalimbali vikiwamo chuo Cha maji,chuo Cha Taifa Cha Zanzibar na Chuo Cha Usimamizi wa Fedha, Watoto 1670 wa miaka 3-5 walipata Elimu ya Makuzi ,Malezi na Maendeleo ya awali, nafasi za kazi zaidi ya 450, Ujenzi wa Madara mapya 22 na Ukarabati wa madarasa 13 pamoja na Walimu 41 wa Elimu ya Awali kutoka Shule za Serikali walipatiwa Mafunzo juu ya Mtaala wa Elimu ya Awali pamoja na kutoa Vifaa vya kufundishia” Alisisitiza Hope
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alilishukuru Shirika Hilo kwa kuwakomboa Mabinti na Wasichana ambao hawakupata Elimu kupitia Mfumo maalumu,
” Niwashukuru Sana kwa Mradi huu ambao unatuachia Urithi mkubwa wa Elimu kwa Watoto wetu, sisi Kama Serikali tunawaomba mkakae chini mtathmini upya Kisha mrudi Tena katika Mkoa wetu wa Tanga na Halmashauri hii ya Jiji la Tanga msiisahau” Alisisitiza Mgandilwa
Alisema Miradi yote ambayo inaachwa na Mradi huo itaendelezwa nakwamba hakuna Mradi hata mmoja ambao utatelekezwa,

” Niwahakikishie kuwa Miradi yote ambayo inaachwa na Mradi huu wa BRAC MAENDELEO TANZANIA itaendelezwa kwa gharama yoyote ile na Serikali itasimamia na kuhakikisha Watoto wetu wanaendelea kupata Elimu” Alisema Mgandilwa
Mwisho








