
Na Boniface Gideon,TANGA
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Salum Nyamwese ,amewaonya wafanyabiashara wanaokwepa kodi kwakutumia njia za panya maarufu kama njia za magendo ,
Nyamwese amesema mfanyabiashara yeyote atakayejaribu kuhujumu uchumi atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Akizungumza jana na Wafanyabiashara pamoja na Wakazi Mkata kwenye uzinduzi WA kituo cha huduma za Kodi cha mamlaka ya mapato TRA Mkoa wa Tanga,
Nyamwese alisema Wilaya ya Handeni ndio lango kuu la usafirishaji wa mizigo na Binadamu katika mikoa ya Kaskazini na Jumuiya ya Afrika Mashariki ,hivyo Wilaya hiyo imeweka mikakati imara ya kiulinzi ili kusitokee mtu atakayekwepa Kodi nakuwataka Wafanyabiashara kufuata Sheria na taratibu za kodi,
” Tunaposema Tanga lango kuu la Uchumi Afrika Mashariki,manake Handeni ndio lango kuu la usafirishaji,hivyo naomba kila mfanyabiashara azingatie taratibu na Sheria za Kodi lakini ukiona kuna jambo halipo sawa basi ni vyema ukaenda TRA mkazungumze lakini ili busara itendeke lakini sio kukwepa kulipa kodi hilo halikubaliki,tunataka kila mfanyabiashara afurahie biashara yake kwakulipa kodi hata ni kidogo kidogo lakini bila kusumbuliwa na mtu” Alisisitiza Nyamwese
Kwaupande wake,Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga,CPA Castro John, alisema kituo hicho cha kodi kitasaidia na kurahisisha Wafanyabiashara pamoja na Wakazi Mkata na maeneo ya jirani kupata huduma zote za TRA na kupunguza umbari mrefu waliokuwa wakisafiri awali kufuata huduma za TRA,
“Kituo hiki cha huduma za kodi Mkata,kinatoa huduma zote za TRA na kinaenda kuwasaidia Wafanyabiashara pamoja na Wakazi Mkata na maeneo ya jirani kupata huduma zote za TRA ,awali wateja wetu walikuwa wakilazimika kusafiri umbari mrefu kufika Handeni mjini kwenda kupata huduma za TRA”Alisisitiza Castro
Castro alisema kwasasa TRA wameongeza mifumo ya huduma ambapo kwasasa wamepata gari maalumu ‘Ofisi inayotembea ‘ nakwamba Wafanyabiashara waliopo maeneo yasiyokuwa naofisi watahudumiwa kama kawaida,
” Kwasasa tumepata gari maalumu ‘Ofisi inayotembea’ ,hivyo tunatoa huduma zote za TRA,kwahiyo wateja wetu ambao wapo mbari na ofisi msijari kabisa tutawafikia Wafanyabiashara wote, lakini pia tunaendelea na kazi ya kuongeza ofisi nyengine katika maeneo mengine yenye umbari mrefu wa mfanyabiashara kufuata huduma za TRA,lengo letu sisi hatutaki Wafanyabiashara watembee umbari mrefu kufuata huduma za TRA ” Aliongeza Castro









