Home Kitaifa NeST YAKATAA MANUNUZI FEKI, TAKUKURU TANGA IKIOKOA MAMILION YA PESA

NeST YAKATAA MANUNUZI FEKI, TAKUKURU TANGA IKIOKOA MAMILION YA PESA

Na Boniface Gideon, TANGA

Taasisi ya kupambambana na kuzuia Rushwa ‘TAKUKURU’ imefanikiwa kuokoa mamilion ya fedha yaliyokuwa kwenye mchakato wa upigaji kupitia ujenzi wa madarasa huku Mfumo wa manunuzi wa kielektroniki (NeST) ukisaidia kuibua dosari katika utekelezaji wa manunuzi hayo.

miradi ya elimu mkoani Tanga na kufungua njia ya kuokolewa kwa zaidi ya Sh milioni 116.2.

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga, Ramadhani Ndwata amewaambia Waandishi wa Habari leo jumatatu Juni 8, 2026 katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya utendaji kazi kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2026 kiasi cha Mil.116.2 ziliokolewa na Taasisi hiyo huku NeST ikigoma kuidhinisha manunuzi hayo ya vifaa vya ujenzi.

Amesema ufuatiliaji wa miradi hiyo umebaini mapungufu yaliyokuwa yakichelewesha utekelezaji licha ya fedha kutolewa.

“Tumebaini dosari kupitia mifumo ya manunuzi na kuchukua hatua mapema, jambo lililosaidia kuzuia upotevu wa fedha za umma,” amesema Ndwata.

Katika Shule ya Sekondari Chongoleani, ujenzi wa madarasa mawili na vyoo ulikuwa umekwama licha ya fedha kutolewa tangu Machi 2024.

Ilibainika kuwa makadirio ya gharama za madarasa yalikuwa chini ya bei ya soko na kufanya zabuni kukataliwa na mfumo wa NeST.

Kwa upande wa vyoo, hakukuwa na maandalizi ya makadirio ya gharama, hali iliyosababisha taratibu za manunuzi kushindwa kuanza kabisa.

“Baada ya kubaini changamoto hizo, tuliimarisha uwajibikaji na sasa mradi unaendelea vizuri,” amesema Ndwata.

Katika hatua nyingine, TAKUKURU ilifuatilia mradi wa Shule ya Sekondari Kwabastola wilayani Muheza wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni moja.

Katika mradi huo, milango ilipakwa varnish, mikanda ya gypsum ikarekebishwa na vitanda 57 kununuliwa vyenye thamani ya Sh milioni 22.4.

“Tunafuatilia pia ukamilishaji wa sakafu, uwekaji wa vigae na ununuzi wa vitanda vilivyobaki ili wanafunzi wanufaike kikamilifu,” amesema Ndwata.

Katika uelimishaji umma, amesema TAKUKURU imewafikia wananchi 189,521 kupitia semina, mikutano ya hadhara, klabu za wapinga rushwa, maonesho na vipindi vya redio.

“Uelewa wa wananchi umeongezeka na ushiriki wao katika mapambano dhidi ya rushwa unaimarika siku hadi siku,” amesema Ndwata.

Kuhusu uchunguzi,Ndwata amesema jumla ya malalamiko 133 yalipokelewa ambapo 100 yalihusu rushwa na mengine kushughulikiwa kwa ushauri au kuhamishiwa taasisi husika.

“Tumefungua mashauri 11 na jumla ya mashauri 18 yanaendelea mahakamani, huku tukihakikisha haki inatendeka,” amesema Ndwata.

Kwa upande wa mikakati ya Aprili hadi Juni 2026,Kamanda huyo wa TAKUKURU amesema wataendelea kuimarisha uelimishaji, uchambuzi wa mifumo na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma.

Ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kuzuia rushwa na kulinda rasilimali za taifa kwa manufaa ya wote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!