Home Kitaifa ZIARA YA MAKAMBA CHUNYA, YALETA FURAHA

ZIARA YA MAKAMBA CHUNYA, YALETA FURAHA

Waziri wa Nishati mhe JANUARI Y.MAKAMBA Leo tarehe 27-07-2022 amefanya ziara wilayani CHUNYA….

Akiwa wilayani CHUNYA, mhe MAKAMBA ambaye aliongozana na mwenyeji wake, mkuu wa wilaya ya CHUNYA mhe MAYEKA S.MAYEKA
Ameongea na wananchi wa wilaya hiyo na kuwahakikishia kupata umeme wa uhakika

Waziri MAKAMBA amezungumza na wanachunya kwenye mkutano wa hadhara, uliofanyika kijiji cha ITUMBI, Kata ya MATUNDASI, wilayani CHUNYA
Amewahakikishia kuwa, vijiji vyote hadi kufikia Dec 2022 vitafikiwa na umeme

Pia ameelezea kuhusu mradi mkubwa wa usambazaji umeme CHUNYA, wenye thamani ya 9.2 bilion unatekelezwa, na kituo kikubwa cha kuongeza nguvu ya umeme “SUBSTATION’ kinaenda kujengwa ili kumaliza tatizo la umeme wilayani CHUNYA

Naye mbunge wa jimbo la LUPA CHUNYA mhe MASACHE KASAKA ameishukuru sana serikali kwa kuendelea kuwa sikiliza na kuyafanyia kazi matatizo na changamoto zinazowakabili

Pia amemuomba mhe waziri, kulitekeleza hilo kwa hima na upesi, ili wanachunya na watanzania waendelee kufaidi matunda ya serikali yao

Pamoja na mbunge, viongozi wa chama cha mapinduzi wakiongozwa na mwenyekiti ndg NOEL CHIWANGA na katibu C.S. JOKEL Pamoja na viongozi wa halmashauri wakiongozwa na mwenyekiti mhe BOSCO MWANGINDE na mkurugenzi mhe TAMIMU KAMBONA wameishukuru sana serikali kwa miradi ya maendeleo inayotekelezwa CHUNYA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!