Home Kitaifa WIZARA YA ARDHI IMEONGEZA SIKU TATU KUSIKILIZA MALALAMIKO YA MIGOGORO YA ARDHI...

WIZARA YA ARDHI IMEONGEZA SIKU TATU KUSIKILIZA MALALAMIKO YA MIGOGORO YA ARDHI DODOMA

Na Magreth Mbinga

Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi imeongeza siku za kusikiliza malalamiko ya migogoro ya Ardhi katika mkoa was Dodoma baada ya siku tano ambazo walipanga kuwasikiliza kuisha na wananchi wengi bado hawajasikilizwa ambapo ilikuwa ni Septemba 26-30,2022 .

Hayo yamezungumzwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mh Allan Kijazi katika mkutano wake na waandishi wa Habari wenyelengo la kuwaarifu wananchi wa Dodoma kujitokeza kutoa malalamiko kwa eneo la Kizota ,Mkuhungu ,Nanara zoezi litaendela Oktoba 17 ,2022 saa mbili mpaka saa kumi jioni wananchi wa maeneo hayo watasikilizwa katika ofisi za Kata za Kizota.

Wananchi wa eneo la Mnadani na Miyuji hawa tutawasikiliza Oktoba 18,2022 kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni naomba wawasilishe malalamiko yao katika Ofisi za kata za Miyui,wananchi wa Mkumba,Chahwa na Ipala watasikilizwa Oktoba 19,2022 katika ofizi za kata za Chahwa” amesema Kijazi.

Pia Kijazi amesema zoezi hili limeongezewa siku tatu kwa Dodoma hii ni kutokana na malalamiko mengi na wananchi baadhi bado hawajasikilizwa lakini pia wameona kwamba kuna haja ya wataalamu wao kabla ya kutoa mrejesho kwa badhi ya malalamiko wapate muda wa kufanya uchambuzi wa malalamiko ambayo yametolewa yafanyiwe uchambuzi.

Hii itatusaidia kuweza kutatua migogoro kwa njia ya haki kwa kila mmoja bila ya kuwa na upendeleo wa aina yeyote na baada ya kumaliza maeneo ya Dodoma tunaendelea na zoezi katika mikoa mingine” amesema Kijazi

Hata hvyo Kijazi amesema kwa upande wa Dar es salaam walipokea malalamiko 386 uchambuzi wa kina ulifanyika baadhi ya malalamiko yalishatolewa uamuzi na mengine yanaendelea kuchambuliwa katika nyaraka mbalimbali katika kumbukumbu zao ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi.

Kwa wale wananchi ambao bado hawajapata mrejesho wasifikilie kwamba malalamiko yao hayakufanyiwa kazi yapo maeneo ambayo tulilazimika kukutanisha watu kama yanahusu pande mbili au tatu tukutanishe ili kuweza kusikiliza hoja ili tuweze kutoa maamuzi sahihi” amesema Kijazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!