Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mhe Mudrik Ramadhan Soraga akizungumzia katika jukwaa la kibiashara baina ya Jumuiya za wafanyabiashara wa Iran na Zanzibar pamoja na Viongozi wa Kiserikali lenye lengo la kubadilishana Uzoefu, Ujuzi na mawazo kwa madhumuni ya kuboresha uhusiano na mazingira bora ya kibiashara baina ya nchi hizo mbili, jukwaa hilo limefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar tarehe 26 agosti 2022.
Jukwa hilo limehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Kiislam ya Iran, wakiwemo Mawaziri na Manaibu Mawaziri, Makatibu na Manaibu Makatibu Wakuu, Mkurugenzi Mtendaji ZIPA, Waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.