Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa Kagera, Mhe. Albert Chalamila ofisini kwake mkoani Kagera.
Pamoja na Mambo mengi, Waziri Bashungwa amempongeza Chalamila kwa kuaminiwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa huo huku akimsisitiza kumusaidia Rais kikamilifu katika kuwahudumia wananchi wa eneo hilo.