Baadhi ya wauza magazeti jijini Dar es Salaam wamelalamikia vitendo vinavyofanywa na askari wa jiji ikiwamo kuchukua meza wanazofanyia biashara hivyo kukwamisha kazi yao wakiomba Rais Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa kuingilia kati kwani wamekuwa wakipata adha huku wakitozwa tozo mbalimbali zinazoipatia serikali mapato.
Ikumbukwe kuwa Oktoba mwaka jana Serikali ilianza kutekeleza mpango wa kuwaondoa wamachinga pembezoni mwa barabara ikiwa ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais Samia la kuwataka wakuu wa mikoa kuwapanga wafanyabiashara hao wadogo ili kuwaondoka katika maeneo yasiyoruhusiwa hasa yaliyopo katikati ya mji.