Furaha na hamasa ya wanasimba leo hii katika kilele cha “Simba Day” ni kuwataka watanzania wote kushiriki katika zoezi la Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kuanza rasmi mnamo tarehe 23 Mwezi huu. #Sensabika #Nguvumoja ndio maneno yanayozungumzwa zaidi hapa kwa Mkapa.
Ni furaha na ndelemo kwa wapenda Soko na wapenda maendeleo wanaojua umuhimu wa maendeleo katika Taifa lao. Ni “Simba Day” ya kipekee kabisa na sasa maalum kuhamasisha mambo ya kimaendeleo.