Home Kitaifa WANANCHI WANAOISHI MIPAKANI WAHAKIKISHIWA USALAMA

WANANCHI WANAOISHI MIPAKANI WAHAKIKISHIWA USALAMA

Na Boniface Gideon, MKINGA

Wananchi wa Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga wamehakikishiwa Usalama wao nakwamba wasiwe na hofu kutokana na kuishi mpakani na Nchi jirani.

Akizungumza Jana kwenye Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kata ya Moa ikiwa ni mwendelezo wa Ziara yake yakutembelea na kukagua kero zakiusalama zinazowakabili Wananchi wanaoishi Mipakani , Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Hamad Masauni alisema Serikali imeimarisha ulinzi na kulipa nguvu Jeshi la Uhamiaji kuwa Jeshi kamili nakwamba wanaanzisha Kitengo maalumu Cha Majini ndani ya Jeshi Hilo ili kupunguza mzigo kwa KMKM.

Serikali imefanya Maboresho ya Sheria ili Uhamiaji liwe Jeshi kamili, Hivyo Sasa hivi Uhamiaji ni Jeshi kamili na tumefungua Chuo huku Mkinga Mkoani Tanga , tunamatumani Wananchi mnatoa Ushirikiano mzuri kuhakikisha mipaka ya Nchi yetu inakuwa salama” Alisisitiza

Masauni alisema Jeshi la Uhamiaji litaanzisha Kitengo maalumu Cha Wanamaji ambacho kitahakikisha Usalama wa Majini unaimarishwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!