Home Kitaifa WAHARIRI WAPIGWA MSASA ELIMU YA AFYA YA AKILI KATIKA KUHABARISHA UMMA

WAHARIRI WAPIGWA MSASA ELIMU YA AFYA YA AKILI KATIKA KUHABARISHA UMMA

Na. Mercy Maimu

Katika kuelekea maazimisho ya afya ya akili duniani, madaktari, wataalamu na wanasaikolojia wameitaka jamii kuepuka msongo wa mawazo kwani ni chanzo kikuu Cha ugonjwa huo.

Wataalamu hao wameyasema hayo leo wakati wa semina maalumu ya wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa maabara ya Taifa uliopo NIMR kwa lengo la kuwaongezea uwezo wa uwelewa wa Afya ya akili kabla ya kuhabarisha jamii.

Msaikolojia Tiba katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Dr Isaac Lema amesema Afya ya akili imegawanyika katika hatua mbalimbali ambazo ni msongo wa mwazo hatua ya kawaida, msongo wa mawazo hatua kati na msongo wa mawazo endelevu.

Afya ya akili ni hali ya ustawi inayomuezesha mtu kuendana na msongo wa maisha,kutambua kazi vyema na kuwa na mchango kwenye afya ya akili. Afya ya akili imegawanyika katika hatua mbalimbali ambazo ni msongo wa mwazo hatua ya kawaida, msongo wa mawazo hatua kati na msongo endelevu.”

Aidha Dk Isaac amegusia malezi kwa wazazi na walezi pia wanaweza kuwa chanzo cha kusababisha afya ya akili kwa watoto au kuwavuruga kama hawatakubaliana namna bora ya malezi kwa ustawi wao.

Naye Mhadhiri wa Chuo Cha Muhimbili Dr Samwel Likindioki amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kutoa elimu kuhusu afya ya akili . Pia amesema majukwaa ya mtandaoni kuchuja habari kabla ya kuziwasilisha kwa jamii ili kuepuka changamoto ambazo zitakazoleta athari kwa watoto na hata watu wazima kupata msongo wa mawazo.

Vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kutoa elimu ila kuna haya majukwaa ya mtandaoni ambayo hayachuji habari kwanza kabla ya kuzipeleka habari Kwa jamii bila kujali madhara yatakayotokea ambayo yataleta msongo wa mawazo katika jamii”.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!