Home Kitaifa WAGONJWA WA HIMOFILIA WAKUMBWA NA CHANGAMOTO ZA KUKOSA FEDHA ZA MATIBABU

WAGONJWA WA HIMOFILIA WAKUMBWA NA CHANGAMOTO ZA KUKOSA FEDHA ZA MATIBABU

Na Magrethy Katengu

Watu wanaosumbumbuliwa na Ugonjwa Himofilia wanakumbana na changamoto ikiwemo gharama kubwa ya matibabu, Madaktari kuchukua muda mrefu kugundua na baadhi ya hospitali kutokuwa na Madaktari bingwa hivyo kupelekea wengine yao kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa maisha.

Akizungumza leo Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Mhimbili Profesa Lawrence Museru wakati akifungua Mafunzo ya siku tatu ya Madaktari kutoka Mikoa mbalimbali ikiwemo Morogoro, Mbeya na Dodoma amesema Ugonjwa huo ni ukosefu wa chembechembe za protini zinazosaidia damu kuganda mwilini lakini watoa huduma huchukua muda mrefu kugundua na ukionekana mgonjwa anakuwa ameathirika kwa kiasi kikubwa hupelekea wengine kupata ulemavu.

Ukiwasikiliza wagonjwa wengi tunaowahudumia wanapitia changamoto mbalimbali kutokana na gharama yake ya matibabu kuwa kubwa tiba nyingine huhitaji milioni 30 kwa mwaka ukizingatia na halihalisi ya kipato cha Mtanzania na hautibiki mgonjwa anapatiwa matibabu maisha yake yote huku akihudhuria kliniki kila baada ya mwezi au mwezi 1-3 wakati mwingine anashindwa kwenda hospitali zilizo katika hospitali ambapo huduma zinapopatikana hivyo wengine hukosa gharama” amesema Prof. Museru
Aidha, Prof Museru alisema kutokana na changamoto ya gharama

kupitia ufadhili wa Mradi wa kuongeza kasi kwa magonjwa ya damu(Novo nordisk haemophilia foundation) umesaidia kusogeza huduma katika mikoa mbalimbali ikiwemo hospitali ya rufaa Mbeya ,Morogoro kwani hapo awali ilikuwa inapatikana katika hospitali ya Taifa Mhimbili tu.

Kwa upande wake daktari bingwa Magonjwa ya damu Stellah Rwezaula amesema Himofilia ni ni ukosefu wa chembechembe za protini zinazosaidia damu kuganda mwilini hivyo asilimia 30 ya watu hupata ugonjwa huu bila kurithi wengine huku asilimia 70 hupata kwa kurithi kupitia vina Saba vya uzazi .

Naye Katibu msaidizi chama cha watu wenye Himofilia Boniface Nzyungu ambaye pia ni Mfamasia alisema yeye ameendelea kuishi na ugonjwa huu na huku akizingatia maelekezo ya Madaktari hivyo ameiomba serikali kufanya kanzidata ya kuwatambua wagonjwa wote katika vituo mbalimbali vya afya nao wanufaike na ufadhili huo wa matibabu kupitia mradi uliojitokeza kufadhili wagonjwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!