Home Biashara WAFANYABIASHARA WA MADINI NZEGA WASEMA MASOKO YA MADINI YAMEBORESHA BIASHARA

WAFANYABIASHARA WA MADINI NZEGA WASEMA MASOKO YA MADINI YAMEBORESHA BIASHARA

Na Boniface Gideon, TABORA

Uongozi wa Soko la Madini Nzega mkoani Tabora umesema kuanzishwa kwa masoko ya madini nchini kumeongeza uwazi, usalama na ufanisi wa shughuli za biashara ya madini.

Akizungumza katika Soko la Madini Nzega, Katibu wa Soko hilo na mfanyabiashara wa madini, Revocatus Chungu, amesema kuanzishwa kwa masoko rasmi kumewasaidia wafanyabiashara kupata maeneo salama na yenye utaratibu mzuri wa kufanya biashara, tofauti na hapo awali ambapo walikosa mifumo thabiti na kukumbwa na changamoto ikiwemo utapeli kutoka kwa watu wa kati.

Ameeleza kuwa kupitia masoko hayo, biashara za madini sasa zinafanyika kwa uwazi zaidi, huku Serikali ikiongeza ukusanyaji wa mapato na wananchi wanaojishughulisha na sekta hiyo wakinufaika na shughuli za madini.

Chungu ameongeza kuwa masoko ya madini yamerahisisha taratibu za biashara, kuharakisha huduma kwa wafanyabiashara pamoja na kuongeza ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa wananchi katika maeneo yanayozunguka masoko hayo.

Kwa upande wake, mfanyakazi wa kampuni ya Banjul Limited, Hussein Sadala, amesema Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tabora imekuwa ikitoa ushirikiano kwa wadau wa sekta ya madini, hali iliyoongeza uwazi na kurahisisha shughuli za biashara.

Amesema uwepo wa masoko ya madini umeondoa changamoto ya kutafuta wateja kwani wanunuzi na wauzaji sasa hukutana moja kwa moja katika soko rasmi, jambo linaloongeza ushindani wa haki na ufanisi wa biashara ya madini nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!