Home Kitaifa VIJANA WATAKIWA KUJITOKEZA TAMASHA LA UTAMADUNI

VIJANA WATAKIWA KUJITOKEZA TAMASHA LA UTAMADUNI

Na Fatma Ally, Dar es Salaam

Waziri wa Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mohamed Mchengerwa amewataka vijana wenye vipaji kujitokeza kuonyesha vipaji vyao kwani Serikali imetenga fungu la kuwasaidia kuviendeleza licha ya kuwapatia tuzo mbalimbali.

Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari wakati alipokua akitolea ufafanuzi juu ya matukio saba yatakayofanyika katika Tamasha la kwanza la utamaduni linalotarajiwa kufunguliwa leo katika viwanja vya uhuru.

Amesema kuwa, tamasha hilo litakuwa la kihistoria na halitamuacha mtu nyuma ambapo kutakuwa na ngoma mbalimbali za asili,vikundi mbalimbali vya muziki ikiwemo Taraabu iliyochezwa hata kabla ya Uhuru na baada na uhuru hivyo ni burudani na vipaji vingi vitatambuliwa na fursa za ajira.

Aidha, amewataka viongozi kuanzia ngazi za Mikoa na Wilaya kuhakikisha nao wanaandaa matamasha ya Utamaduni katika maeneo yao ili kusaidia kuenzi fikra za Waasisi wa Taifa .

Hata hivyo, amesema miongoni mwa matukio yatakayofanyika katika Tamasha hilo ni kufanya maandamano ya amani kutoka Temeke hadi uwanja wa uhuru ambapo mgeni rasmi atakua ni Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chisano.

Aidha amewataka wananchi wote kuhudhuria kujifunza mengi kwani ifikapo julai 7 mwaka huu Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya siku ya kiswahili duniani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!