Home Kitaifa UTARATIBU UGAWAJI FEDHA MATUMIZI MFUKO WA JIMBO MUSOMA VIJIJINI WAPONGEZWA

UTARATIBU UGAWAJI FEDHA MATUMIZI MFUKO WA JIMBO MUSOMA VIJIJINI WAPONGEZWA

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI na wadau wa elimu jimbo la Musoma Vijijini wamepongeza utaratibu mzuri wa kufanyika vikao vya ugawaji matumizi fedha za mfuko wa jimbo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mzawa Blog wamesema utaratibu unaofanyika Musoma Vijijini hawajausikia sehemu nyingine.

Wamesema kila fedha zinapo patikana mbunge huitisha kikao cha wajumbe wa fedha za mfuko wa jimbo na kupitia maombi kutoka kwenye Kata na kufanya mgao.

Juma Lukiko mkazi wa Rukuba amesema ameona taarifa ya mgao wa fedha za mfuko wa jimbo na namna zilivyoelekezwa kwenye miundombinu ya elimu na kupongeza utaratibu huo.

Amesema katika mgao aliouona shule ya sekondari Rukuba imepata mgao wa bati 106 na nondo 30 katika ukamilishaji wa sekondari yao.

Juma amesema sekondari zilizo kwenye ukamilishaji,ujenzi na zilizo tayari kwa ujenzi zimepata mgao wa fedha kuinua sekta ya elimu.

” Tunampongeza mheshimiwa mbunge kwa utaratibu mzuri wa uwazi kwenye matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo.

” Elimu ni kipaumbele kwenye jimbo letu na tunaona namna ambavyo fedha zimeelekezwa huko kutokana na vikao”,amesema.

Jumla ya shilingi milioni 75,796,000 za mfuko wa jimbo zimeelekezwa kununua vifaa vya ujenzi zikiwe saruji,nondo na rangi kwaajili ya miundombinu ya elimu jimbo la Musoma Vijijini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!