
Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amekamilisha ahadi yake ya kuwezesha waendesha pikipiki” bodaboda” kupata mkopo nafuu wa pikipiki.
Hiyo ni ahadi aliyoitoa wakati akifunga mafunzo ya udereva aliyowezesha chuo cha ufundi Veta Mara hivi karibuni kwa bodaboda wa Musoma mjini ambao walikuwa hawajapitia mafunzo ya udereva.
Akizungumza kabla ya kukabidhi pikipiki hizo kwa waliokamilisha taratibu akiwa ameambata na viongizi mbalimbali akiwepo mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amesema amefurahi kuona jambo hilo linakwenda vizuri.
Amesema mpango huo umepokelewa na unakwenda vizuri kwa kupata pikipiki kwa kutanguliza laki 3 na kulipa kidogo kidogo kwa miezi 11 muhusika anamiliki pikipiki.

Mathayo amesema zipo njia nyingi za kumsaidia mwananchi na vijana kujiinua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kupata mikopo nafuu na kujiepusha na kausha damu.
Amesema kupitia ofisi ya bodaboda Wilaya ya Musoma wameanza kuwezesha vijana kupata pikipiki ambazo hazita waumiza kichwa marejesho yake.
” Niwapongeze wale waliokuwa tayari kwa kukamilisha taratibu ikiwa ni pamoja na kutanguliza kiasi cha shilingi laki 3 pekee na kupata pikipiki.
” Ofisi nimewawekea hapa mratibu wa ofisi namlipa mshahara kula mwezi fikeni mpewe taratibu mwenye kuhitaji aweze naye kuipata”,amesema

Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amempongeza mbunge huyo kwa jitihada zake za kuwafikia vijana na kuwawezesha kiuchumi.
Amesema waliopata pikipiki hizo wazitumie vizuri na kuhakikisha miezi 11 ikikamilika wanakuwa wamiliki wa pikipiki
Juma Nyangi mkazi wa Kanyonge mmoja wa waliopata pikipiki amemshukuru mbunge Mathayo kwa kufanikisha kupata pikipiki ya mkopo nafuu.
