Home Kitaifa KILANGO AENDELEA KUIMARISHA MIUNDO MBINU YA BARABARA JIMBO LA SAME MASHARIKI ATOA...

KILANGO AENDELEA KUIMARISHA MIUNDO MBINU YA BARABARA JIMBO LA SAME MASHARIKI ATOA SHUKRANI KWA MUNGU.

Na Dickson Mnzava,

Ujenzi wa Barabara 100.5Km Mkomazi-Kisiwani-Same waanza, Mkandarasi wa Ujenzi wa Kipande cha 36 Km cha Mkomazi – Ndungu akabidhiwa Barabara Ujenzi kuanza rasmi.

Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Mhe. Anne Kilango Malecela ameshiriki katika Ibada na Waumini wa Kanisa la KKKT Usharika wa Ndungu na kutoa Sadaka ya Shukrani katika Kanisa hilo kwa Kumshkuru Mungu kwa matendo makuu ambayo amemtendea ikiwemo kufanikishwa kwa Makabidhiano na Mkandarasi wa Ujenzi wa kipande cha Barabara ya Mkomazi – Ndungu (Km 36) kwa Kiwango cha lami.

Awali, akizungumza na Waumini wa Kanisa hilo Mhe. Kilango amesema amewiwa kusogea mbele za mwenyezi Mungu kumshukuru kwaniaba ya wananchi wa Jimbo hilo la Same mashariki kwa makuu ambayo Mungu ameendelea kuwatendea wananchi wa jimbo hilo akisema yote yaliyofanyika chini ya uongozi wake ni neema tu ambayo Mungu amewapa.

“Nimewiwa kusogea madhabahuni hapa kumshukuru Mungu kwa kile alichotutendea katika Jimbo letu na Wananchi wangu wa Same Mashariki, kwani kilio cha Barabara hii nicha muda mrefu na leo Mungu amekisikia na hatimae Ujenzi wa Barabara ya Mkomazi – Kisiwani – Same kwa kiwango cha lami unaanza”.
“Alisema Kilango “.

Aidha ameendelea kuwasihi waumini na viongozi wa dini mbalimbali ndani ya Jimbo hilo kuendelea kuombea amani na utulivu ndani ya Jimbo hilo sambamba na kuendelea kuliombea Taifa la Tanzania amani chini ya utawala mahiri wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!