Na.Khadija Seif, Mzawablog
KATIKA kuunga mkono jitihada za serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan Kanisa la RGC Miracle Centre linatarajia kufanya tamasha la muziki wa Injili Disemba mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo lenye lengo la kulimobea taifa amani na upendo pamoja na kumuombea dua Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza Dar es Salaam Mkurugenzi wa kanisa hilo, Nabii Peter Nyanga alipokuwa anazindua Tv ya kanisa hilo iitwayo ‘Urejesho’ amesema wana mpango wa kufanya tamasha kubwa ambalo litakuwatanisha watu wengi ikiwemo wahubiri mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
“Tumeanza na jambo la kuzindua televisheni yetu ambayo itakuwa inaonyesha mambo mbalimbali katika nchi 34 za Afrika, ila Disemba tuna mpango wa kufanya tamasha kubwa la nchi.“
Aidha, Nyanga amesema wanahitaji tamasha hilo liwe kubwa ili kuliombea taifa pamoja na Rais Samia kutokana na mambo makubwa anayoyafanya.
“Nimefungua televisheni hii kutokana na kipindi cha uviko 19 mwaka 2020 nilipata tabu katika suala la kutoa mahubiri kwa wananchi hivyo ikatulazimu tutafute njia sahihi ya kufikisha neno la kiroho Kwa njia ya televisheni.”