Home Kitaifa UMMY MWALIMU APOKEA VIFAA KINGA NA NYENZO ZA KUTOLEA ELIMU

UMMY MWALIMU APOKEA VIFAA KINGA NA NYENZO ZA KUTOLEA ELIMU

Kyerwa, Kagera

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo amepokea vifaa kinga na nyenzo za kutolea elimu kwa umma kutoka Shirika la MDH-Tanzania ikiwa ni utayari wa kukabiliana na tishio la ugonjwa wa Ebola.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa katika soko la Kimatifa la ndizi lililopo Murongo ambapo ni Mpakani mwa Tanzania na Uganda na Meneja wa Ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kutoka MDH Dkt. Boniphace Jullu kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Dkt. David Sando

Waziri Ummy amewashukuru MDH kwa msaada huo ambao ameukabidhi kwa Uongozi wa Mkoa wa Kagera kupitia Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Rashid Mwahimu.

Vifaa vilivyopokelewa ni pamoja na Vipima joto ( Thermoscanner), Vitakasa mikono (Sanitaizer), Barakoa, ndoo za kunawia mikono, vipaza sauti( Mega phones) pamoja na mabango na vipeperushi kwa ajili ya kutolea elimu na uhamasishaji kwa jamii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!