Na Magrethy Katengu
Mamlaka ya hali ya Hewa TMA imetoa utabiri wa hali ya hewa unaonyesha Vipindi vya Upepo mkali unafikia Kilometa 40 kwa saa huku Mawimbi makubwa yanayofikia Mita 2.0

Pia Utabiri huo unaonyesha Vipindi hivyo vinatarajiwa katika baadhi ya Maeneo ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga (ikijumuisha Visiwa vya Mafia, Dar es salaam,na Visiwa vya Unguja na Pemba.
Aidha Matarajio kwa siku ya Jumatatu ya tarehe 06/3/2023 kutakuwa na mabadiliko kidogo.









