Wizara ya Fedha na Mipango imekanusha taarifa ya uzushi na upotoshaji iliyochapishwa na mtandao wa kijamii wa Tanzania Abroad TV kuhusu madai ya Tanzania kudaiwa kiasi cha zaidi ya Trilioni 10 na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB).
Taarifa kutoka Wizara ya fedha na Mipango imesisitiza kitendo hicho kuwa ni uzandiki na kinaleta taharuki katika jamii, hatahivyo wizara imetoa wito kwa jumuiya za kimataifa na watanzania kupuuza Taarifa hiyo yenye upotoshaji mkubwa.









