Home Kitaifa TIGO NA XIAOMI WAZINDUA SIMU HII KALI

TIGO NA XIAOMI WAZINDUA SIMU HII KALI

Na Mwandishi Wetu

• Wateja kupata hadi GB 66 za intaneti kutoka TIGO bila malipo kwa mwaka mzima.

Dar es Salaam. Tarehe 25 Oktoba, 2022. Kampuni inayoongoza katika utoaji wa huduma za kidijitali nchini, Tigo Tanzania, imeshirikiana na XIAOMI Tanzania kuzindua XIAOMI REDMI A1 PLUS itakayouzwa kwa Sh 225,000 kwa bei ya rejareja. Uzinduzi huo unaifanya Tigo Tanzania kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiliano ya simu kuachia simu hiyo nchini baada ya uzinduzi wa kimataifa.

XIAOMI REDMI A1 PLUS inawahudumia watumiaji wote wa simu mahiri kwa mara ya kwanza zenye umaridadi, na za kisasa zaidi.

Simu hizi zinawahakikishia wanunuzi utendakazi wa hali ya juu, alama za vidole ( finger print ),  upigaji picha wa hali ya juu kupitia usanidi wa kamera mbili na kamera ya selfie ya pembe pana, na betri inayoweza kukaa hadi siku nzima.Akizungumza baada ya kutangaza simu hizo , Meneja wa bidhaa za Intaneti kutoka Tigo, Bi. Imelda Edward amesema
 “Tunapoendelea kutumia nguvu ya ushirikiano wetu kuunganisha watanzania na huduma za kidijitali, ninafurahi kwamba simu hizi zitafungua uwezo kwa wateja wengi zaidi kupata mtandao wetu wa 4G ambao unaongoza zaidi hii ikiwa ni mkakati wa kupenyaza simu mahiri  kwa watanzania ili kutupeleka kwenye nafasi nzuri  ya watumiaji wa kidijitali na data”.
“Wateja wa Tigo watafurahia matumizi bora ya kidijitali kupitia mtandao wa kasi zaidi wa 4G+ ambao ni mkubwa zaidi nchini, tunatoa GB 66 za intaneti BURE kwa mwaka mzima kwa wateja wote watakaonunua XIAOMI REDMI A1 PLUS.” katika maduka yetu ya Tigo na XIAMI nchini alimalizia. Naye kwa Upande wake Meneja Masoko  kutoka XIAOMI Tanzania Alex Katagira,amesema kuwa 
“Uzinduzi wa A1 Plus ni mwendelezo wa ushirikiano wetu na Tigo, lengo letu kuu ni kuwapa wateja wetu simu mahiri ambazo ni rafiki kwa mtumiaji, A1 Plus ni simu mahiri yenye uwezo wa kumudu 4G bora na yenye sifa nzuri, yenye kamera mbili, muundo bora, alama za vidole ( finger print ),  5000mAh betri kubwa (kuchaji kwa haraka waW 10) RAM kubwa ambayo pia inaweza kuongezwa ” Alimalizia
Wateja wa Tigo wanaweza kupata simu hii mpya ya kisasa kutoka kwa duka lolote la Tigo kote nchini. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!