Home Kitaifa TANZANIA NI MAHALI SALAMA KWA BIASHARA NA UWEKEZAJI

TANZANIA NI MAHALI SALAMA KWA BIASHARA NA UWEKEZAJI

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bi. Pendo Godwe amesisitza kuwa tanzania ni sehemu sahihi ya kuwekeza kwa wawekezaji wa ndani na nje, amebanisha hayo katika Maonesho ya SabaSaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam na kuwaomba wawekezaji wasisite kuja kuwekeza katika fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya nchi ya Tanzania katika sekta za utalii, kilimo, elimu, viwanda nk

Tunahamasisha watanzania zaidi waje kuwekeza kwenye kilimo na wageni ambao wanania ya kuwekeza ambao wameshiriki katika maonesho haya ya sabasaba” – alisisitiza

Aidha, katika kurahisisha huduma zake kituo cha uwekezaji Tanzania kimefanikiwa kuwa na mfumo wa utoaji huduma wa panoja ambao unaunganisha taasisi zaidi ya 12 zinahusisha masuala ya kibiashara na uwekezaji, Pendo alifafanua “TIC inatoa huduma chini ya Mahala pamoja mpaka sasa tuna taasisi zaidi ya 12 ambazo ziko ndani ya TIC ikiwemo BRELA, TRA, NIDA, OSHA, TBS, UHAMIaJI, IDARA YA KAZI, ARDHI NA TANESCO”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!