Home Kitaifa TAKUKURU KUCHUNGUZA MIRADI YA AFYA MANISPAA YA SUMBAWANGA

TAKUKURU KUCHUNGUZA MIRADI YA AFYA MANISPAA YA SUMBAWANGA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akisalimiana na wananchi wa mtaa wa Mponda leo alipokwenda kukagua mradi wa ujenzi wa zahanati yao iliyoanza kujengwa mwaka 2013 ambapo ameagiza ikamilike mwanzoni mwa mwaka 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akizungumza na watalaam wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Matanga leo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akiongea na akina mama waliofika katika eneo la mradi wa ujenzi wa hospitali ya Isofu Manispaa ya Sumbawanga keo alikagua mradi huo ambapo amewahakikishia kuwa mapungufu yatatauliwa ili ianze kazi ya kuhudumia wananchi.
Meneja wa RUWASA Rukwa Mhandisi Pius Boaz akitoa maelezo kuhusu mradi wa maji Mponda kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa leo ambapo amewataka wananchi kuchangia kwa wakati bili za maji ili kulinda miundombinu .
Sehemu ya majengo ya kituo cha Afya Mollo ambayo yamegahrimu shilingi Milioni 400 lakini mengine bado hayajakamilika hatua iliyomfanya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga kuagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi.

Na. OMM Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga ameagiza  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  kufanya uchunguzi wa haraka juu ya miradi ya ujenzi wa vituo vya afya na hospitali katika Manispaa ya Sumbawanga ili kuona endapo kuna matumizi mabaya ya fedha za umma.

Kauli hiyo ameitoa leo (Ijumaa Oktoba 21, 2022) wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa kituo cha afya Mollo, zahanati ya Nambogo, kituo cha Afya Matanga, hospitali ya wilaya iliyopo Isofu na zahanati ya Mponda ambapo hakuridhishwa na namna miradi hiyo ilivyochelewa kukamilika.

Mkuu huyo wa mkoa alimwagiza Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Sumbawanga James Mbungano kuwasilisha taarifa ya kina Jumatatu ijayo (24 Oktoba, 2022) juu miradi hiyo na hatua walizochukua tangu ilipoanza kutekelezwa.

Kwa mujibu wa taarifa za Halmashauri hiyo gharama za vituo hivyo kwenye mabano kituo cha Afya Mollo (Milioni 400), Matanga (Milioni (500), Isofu (Bilioni 1.8) na Mponda (Milioni 80)

Wajibu wetu ni kusaidia kazi katika maeneo ambayo Rais Samia Suluhu Hassan hawezi kufika .Sisi viongozi wa mkoa na wilaya tutumie nafasi zetu kutakua kero za miradi ya afya ili wananchi wapate huduma” alisisitiza Sendiga.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba alisema atahakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kuwa atahakikisha fedha za serikali zilizotolewa zinaleta matokeo chanya.

Naye Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Jastin Malisawa akizungumza kuhusu kuchelewa ujenzi wa zahanati iliyoanza mwaka 2013 kutokamilika alisema halmashauri itatoa fedha na kuwa zahanati hiyo itakamilika mapema mwaka 2023.

Ombi langu tutatoa shilingi Milioni 25 ili ifikapo mwezi Februari 2023 tukamilishe na kuanza kutoa huduma za afya kwa wananchi wa Mponda” alisema Mstahiki Meya Malisawa.

Mkuu wa Mkoa huyo wa Rukwa yuko kwenye ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na serikali kwa upande wa sekta wa sekta ya afya ili wananchi wapate huduma za afya karibu na maeneo yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!