Home Kitaifa TAASISI ZA FEDHA NCHINI ZAHIMIZWA KUTOA MIKOPO YENYE RIBA NAFUU KWA WAJASIRIAMALI

TAASISI ZA FEDHA NCHINI ZAHIMIZWA KUTOA MIKOPO YENYE RIBA NAFUU KWA WAJASIRIAMALI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ahimiza taasisi za Fedha Nchini kutoa mikopo yenye riba nafuu Kwa wajasiriamali.

Mhe. Kijaji ameyasema hayo tarehe 17 Novemba, 2022 alipofanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA (United Bank for Afrika) Bw. Oliver Alawuba na kujadiliana masuala ya kukuza Biashara Nchini hasa katika huduma za kifedha ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu kwa wajasiriamali kuanzia wadogo hadi wakubwa.

Katika wakati mwingine Dkt. Kijaji tar 17 Novemba, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya KIOO limited Bw. Kumar Krishnan.

KIOO Limited ni watengezaji na wasambazaji wa vifungashio vinavyotumika kufungasha bidhaa mbalimbali.

Bw. Kumar amemueleza Waziri wa Uwekezaji kuwa wamedhamiria kufanya upanuzi wa kiwanda kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa chupa kwa ajili ya kusafirisha Nje ya Nchi. Uwekezaji huo utakaogharimu dola za Kimarekani Milioni sitini (60) na unaenda kuongeza ajira ya watanzania 250 hivyo kiwanda hicho kufikisha ajira ya watu mia tisa (900).

Bw. Kumar amesema kuwa wanaendelea na mazungumzo na TIC kwa ajili ya Uwekezaji wa kiwanda cha Sukari Songea Mkoa wa Ruvuma ambao unaenda kuajiri wafanyakazi zaidi ya elfu kumi (10,000).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!