Home Kitaifa SHIVYAWATA BUKOBA WASHIRIKI SHEREHE ZA UHURU, WATAJA MAFANIKIO NA KUPONGEZA SERIKALI

SHIVYAWATA BUKOBA WASHIRIKI SHEREHE ZA UHURU, WATAJA MAFANIKIO NA KUPONGEZA SERIKALI

Na Theophilida Felician, Kagera.

Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania SHIVYAWATA Manispaa ya Bukoba Mkaoani Kagera wameungana na wananchi wengine nchini kushiriki sherehe za Uhuru wa miaka 62 kwakuyataja mambo mbalimbali yamafanikio juu ya watu wenye ulemavu.

Wakizungumza na Blog hii ya Mzawa ofisini kwao Manispaa ya Bukoba viongozi wa shirikisho hilo hii leo Tarehe 9, Desemba mwaka huu wa 2023 wamesema kwamba leo ikiwa ni siku ya kusherekea Miaka 62 tangu Tanzania ipate Uhuru wamefarijika kuona wanasherehekea Uhuru huo ulioyajaza mafanikio tele tangu kupatika kwake.

Viongozi hao wakiambatana na Mwenyekiti wao ambaye ni mtu mwenye ulemavu wakutokuona Novati Joseph Mwijage wameeleza kuwa serikali imekuwa ikipiga hatua siku hadi siku katika kutambaua makundi ya watu wenye ulemavu kwa namna mbalimbali kuliko miaka ya kipindi cha nyuma.

Mwenyekiti huyo awali amefafanua kuwa serikali kwa Mkoa Kagera mwaka 1966 ilianzisha shule ya msingi Mgeza mseto ambayo imewasaidia watu wengi wenye ulemavu.

Ameeleza kuwa baada serikali kuendelea kuweka miundo mbinu wezeshi baadhi ya shule jamii imekuwa na mwamko wa kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu.

Pia amegusia suala la uwepo wa mpango wa elimu jumuishi ambao kwa namna moja au nyingine umeongeza kiwango cha watoto kupata elimu japo bado siyo kwa kiwango kikubwa.

Jambo jingine amelitaja la mikopo ya 2% inayowalenga wao mikopo ambayo waliowengi hawajaweza kunufaika nayo vizuri.

“Miaka hii 62 ya Uhuru tunatoka sehemu tunasogea sehemu japokuwa watu wenye ulemavu bado hatujawasilishwa rasimi kwenye vyombo vya kutolea maamzi mfano kwenye Kitongoji, Kijiji, Kata, kwenye Bunge labda yawezekana wakawepo watu waviti maalumu lakini huku chini, chini ya mzizi hatuna wakutusemea nabaadhi ya mambo yetu yanasahaulika kwa sababu hatuna wa wakirishi ” amesema Novati Joseph.

Kitu cha kwanza tumeangalia awamu hii ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwakuonyesha kwamba sasa anaomwelekeo wakuanza kuwagusa watu wenye ulemavu mfano ameanza kuwabaini wenye vipaji, lakini pia linapotokea jambo linalotuhusu sisi mama akiipata habari analitatua liwe nila kijamii, kiuchumi, hata kisiasa” ameendelea kutoa ufafanuzi Novati.

Hata hivyo amesema kuwa mahitaji yao ni suala mtambuka mfano kwa upande wa afya, Elimu, uchumi hivyo serikali na wadau hawana budi kuongeza juhudi ya kuwatambua na kuwasaidia kwa namna tofauti tofauti.

Ametoa shukrani na pongezi kwa serikali akisema kuwa wanapoelekea yawezekana changamoto walizo nazo zitapatiwa ufumbuzi kutoka na jitihada zinazoonyeshwa na serikali dhidi ya kundi hilo.

Sambamba na hayo amewasihi watu wenye ulemavu kujitambua na kujikubali kutokana na hali zao, kuinuka na kupaza sauti ili wasisahaulike, mwisho kabisa akiwaomba na wadau kujitokeza katika kuendelea kuwaunga mkono kwa mambo kadha wa kadha.

Deliphina Joseph ni mtu mwenye ulemavu wa ukiziwi yeye licha yakuyataja mafanikio amezitaja na changamoto zinazowakabili wao hasa hasa pale wanapokuwa wakihitaji huduma ofisi yoyote hukwama kutokana na kutokuwepo kwa wakalimani wakuwasaidia mawasiliano sahihi kati yao na watoa huduma.

Deliphina akisaidiwa na Sweetbati Mushana kuelezea maoni yake hayo amebainisha kuwa ofisi nyingi hazina watu wenye utalaamu wa Lugha za alama ambapo ametolea mfano wanapokwenda Hospitalini au kituo chochote cha kutolea huduma za afya huwapa wakati mgumu wakuweza kuelewana na madakitari jambo ambalo huwapelekea pengine kushindwa kuamini kuwa dawa walizohudumiwa ni sahihi.

“Mfano mwingine ni kwenye shughuli za mikutano ya kijamii iwe ya viongozi wakubwa huwezi kumkuta mkalimani wakutusaidia hata sisi tukaelewa kinachozungumziwa pale hata kama kina tuhusu hivyo hujikuta tukishiriki mikutano hiyo bila kujua kitu licha yakuhudhuria, tukijakufahamu unakuta jambo lililoongelewa limeishapita muda kwakweli hii bado nishida mno” Deliphina akizungumza bayana.

Ameiomba Serikali kuona namna ya kusaidia katika kuitatua changamoto hiyo japo kwa kiwango chake huku akitoa na ushauri kwamba ione haja ya kupanua wigo wakuanzisha mitaala ya elimu ya lugha za alama kuanzia ngazi za shule za msingi ili kuweza kuibua watalaamu wengi wa namna hiyo kwa malengo ya kukidhi mahitaji ya watalaamu hao.

Kwa pamoja viongozi hao kutoka CHAVITA, CHAWATA, TCB, TAS, na TAMAH wa meleezea changamoto ya upatikanaji wa nyenzo za vifaa muhimu vya kuwasaidia vimekuwa changamoto kubwa kupatikana maana vinauzwa kwa bei ghali na havipatikani Mjini Bukoba mfano magongo, fimbo pamoja na mafuta ya kujipaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Ualbino)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!