Home Kitaifa SHILINGI BILILONI 93.6 ZIMELIPWA KWA MKANDARASI WA UJENZI WA KITUO CHA KUPOZA...

SHILINGI BILILONI 93.6 ZIMELIPWA KWA MKANDARASI WA UJENZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME CHALINZE

Na Scolastica Msewa, Chalinze
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha kupoza Umeme cha Chalinze mkoani Pwani ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 93.7 na tayari shilingi bilioni 93.6 zimekwishalipwa kwa Mkandarasi wa Kituo hicho kati ya shillingi Bililoni 158 za gharama za mradi wote.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Kilumbe Ngenda wakati kamati hiyo ilipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Kituo cha kupoza Umeme cha Chalinze ambacho hupokea Umeme kutoka katika Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Julias Kambarage Nyerere la wilayani Rufiji.

Alisema Kamati hiyo imefurahishwa na hatua za Maendeleo ya ujenzi wa mradi huo iliyofikiwa baada ya kukagua hatua zote ikiwa ni pamoja na eneo la mitambo ya kupokea Umeme kutoka Bwawa la Mwalimu Nyerere na eneo la mitambo ya kupoza umeme, transfoma sita zilizofungwa na kazi ndogo ndogo zinazoendelea kukamilisha ujenzi huo.

Alisema maendeleo na jitihada za ujenzi wa mradi huo zinafanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa hatua kubwa hadi sasa mradi umefikia asilimia 93.7 kwani yeye ndio Mkuu wa nchi na Maendeleo ya ujenzi wa mradi huo unafanyika chini ya Utawala wake.

“Niwapongeze kwani kazi iliyofanyika ni kubwa sana kutoka asilimia 55 tuliyoikuta awamu iliyopita na Sasa mradi umefikia asilimia 93.7 ambapo pia Kuna baadhi ya majengo yamekamilika kwa asilimia 100 mfano ni jengo la kuendeshea mitambo na kusema kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM chama ambacho kimekuwa kikiahidi na kutekeleza ahadi zake kwa wananchi” alisema.

Alisema kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho cha kupooza umeme cha Chalinze ni hatua nzuri kwa taifa kwani kitachochea kutimia kwa sera ya taifa ya Tanzania ya viwanda na uwekezaji kwani hakuna viwanda bila umeme.

Naibu waziri wa Nishati na Madini Judith Kapinga ameshukuru kwaajili ya kamati hiyo kutembelea mara kwa mara kukagua mradi huo wenye maslahi mapana kwa taifa ili kuona utekelezaji wake waweze kushauri na kuelekeza namna bora ya utekelezaji wa miradi hiyo ambayo inagharimu fedha nyingi sana.

“Nataka tuihakikishie kamati na Mheshimiwa spika wa bunge kwamba maelekezo ya kamati na mapendekezo yote tunayapokea kwa weledi mkubwa sana na kuhakikisha tunafanyia kazi ili kuhakikisha miradi hii yenye tija kubwa sana kwa taifa inaendelea kutekelezeka vizuri”.

“Lakini kipekee niseme miradi hii imetekelezwa katika awamu ya sita ilianza katika awamu hii ya sita ambapo tunapomaliza miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tunayo miradi ya kujivunia, miradi ya kielelezo na ina maslahi makubwa kwa taifa letu na ipo katika hatua za mwisho ili kukamilika”

Njia ya kusafirisha umeme ni mradi ulianza kujengwa mwezi julai 2021 na kituo cha kupooza umeme kilianza kujengwa mwezi oktoba 2021 ambapo kimefikia asilimia 93.7 ya ujenzi wake yaani ni miradi iliyoanaza na awamu ya sita ambapo miradi hii yote miwili imeshafikia asilimia 99.5 ya ujenzi wake na inakalibia kufika ukingoni alisema Judith.

“Tayari shilingi bilioni 93.6 zimekwishalipwa kwa Mkandarasi wa Kituo hicho kati ya shillingi Bililoni 158 za gharama za mradi wote hadi kufikia tarehe 30 mwezi uliopita”.

“Watanzania tumeshaanza kuona matunda ya Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Julias Kambalage Nyerere na tunaendelea na utekelezaji wa mradi huo na tunahakika ya kwamba tutakamilika kwa wakati kwamba mradi unaenda vizuri na tutaendelea kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa Watanzania”.

Hatahivyo alisema changamoto iliyopo kwasasa ni changamoto ya miundombinu kwa baadhi ya maeneo ni chakavu na ya siku nyingi ingawa serikali inaendelea kulifanyia kazi kwa wakati ili umeme uweze kufika vizuri.

Awali akitoa taarifa ya maendeleo ya Meneja wa Mradi Newton Livingstone alisema Mkandarasi anaendelea na Kazi za ujenzi wa miundombinu ya Kituo hicho ikiwa ni pamoja na Barabara, nyumba za Wafanyakazi na ghala la kuhifadhia mitambo ambapo kazi hizo haziathiri uendeshaji wa Kituo hicho.

Newton alisema tayari ujenzi wa miundombinu wezeshi ili kusafirisha na kupoza Umeme unaotoka Bwawa la Mwalimu Julias Kambarage Nyerere la Rufiji kuja Chalinze umekamilika na megawati 235 zinaingia kwenye gridi ya Taifa kupitia Kituo hicho na kufanikiwa kumaliza mgao wa Umeme nchini.

Afisa uhusiano huduma kwa wateja Tanesco mkoa wa Pwani Esta Msaki amewataka wananchi katika maeneo mradi huo ulikopita waendelee kulinda na kutunza miundombinu ya mradi huo ili iwe endelevu kwani wapo ambao huaribu miundombinu kwa makusudi na wengine kwa kutokujua.

Huu mradi serikali imewekeza kwa asilimia 100 kutoka pesa za watanzania hivyo ni mradi wa watanzania hivyo tuendelee kutunza na kulinda miundombinu yetu ili tuendelee kupata umeme wa uhakika alisema Esta.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!