Home Kitaifa SHAKA HAMDU SHAKA ATEMBELEA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE, MUHIMBILI

SHAKA HAMDU SHAKA ATEMBELEA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE, MUHIMBILI

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka amefanya ziara katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo akiwa kwenye ziara hiyo amepata nafasi ya kupokea taarifa zinazohusu taasisi hizo.

Aidha Shaka amepata nafasi ya kuzungumza na Wananchi mbalimbali waliokuwa wakipatiwa huduma mbalimbali.Pia katika ziara hiyo amezungumza na baadhi ya raia wa nchi mbalimbali za Afrika wakiwemo wa Rwanda,Burundi na Congo ambao wamekuja kupata huduma za matibabu ya afya.

Shaka amefanya ziara hiyo jana mchana na lengo la ziara yake pamoja na mambo mengine ilikuwa ni kwenda kumjulia hali mzazi wa Watoto mapacha waliotengenishwa Amina Amosi(18) Mkazi wa Simiyu aliyepo Hospitalini hapo.

Amemtia moyo huku akitoa maelekezo kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii kutembelea mzazi huyo na kumueleza namna ambavyo Serikali itamsaidia malezi ya Watoto.

Akiwa katika ziara hiyo Shaka amepokea taarifa ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba pamoja na uwekezaji katika miundombinu.

Aidha Shaka ameeleza mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha sekta ya afya huku akizungumza mipango ya kuijenga Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo zaidi ya Sh.bilioni 600 zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo ambao unakwenda kuandika historia nyingine katika sekta ya afya nchini.

Hata hivyo amewapongeza watoa huduma katika taasisi hizo kutokana na huduma bora ambazo wanazitoa katika kuwahudumia Wananchi huku akieleza kwamba Kuna mambo makubwa na mazuri yamefanyika tofauti na baadhi ya watu wanavyozungumza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!