Home Kitaifa SERIKALI IMEKUJA NA MAJIBU YA MALALAMIKO YALOYOWASILISHWA NA MADEREVA PAMOJA NA VYAMA...

SERIKALI IMEKUJA NA MAJIBU YA MALALAMIKO YALOYOWASILISHWA NA MADEREVA PAMOJA NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI

Na Magreth Mbinga

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi ,Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu yenye dhamana ya ajira na kazi imefanyia kazi hoja ambazo zilitolewa na pande zote mbili na kusema Serikali inaendelea kufanya kaguzi zinazoshirikisha wadau wa sekta hiyo ili kuhakikisha madereva wanapata mikataba ya kazi.

Hayo yamezungumzwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye ulemavu Mh Potras Katambi na kusema kuwa katika hatua za awali ukaguzi ulifanyika katika mikoa ya Dar es Salaam,Arusha,Mwanza,Pwani na Mbeya ambapi jumla ya kampuni 73 yalikaguliwa na kugundua waajiri hawajatoa mikataba kwa madereva.

Kutokana na hali hii Serikali imetoa maelekezo ya kisheria ili kuwataka waajiri kutoa mikataba ya wafanyakazi na madereva zoezi la ukaguzi ni endelevu na kama nilivoeleza Juni 11 mwaka huu na nilizungumza kwamba ifikapo Agosti mwiahoni mwaka huu Serikali itaanza kuchukua hatua kwa waajiri ambao watabainika kukaidi maelekezo ya Serikali“amesema Mh Katambi.

Aidha Mh katambia amessma kupitia kaguzi zinazoendelea kufanyika katika maeneo ya kazi Serikali itasimamia swala madereva kupatiwa hati ya malipo ya mshahara kama inavyo elekezwa na sheria.

Pia Mh Katambi amesema Serikali itaendelea kuitisha vikao hivyo kama sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya kawaida bila kusubiri kuibuka kwa migogoro .

Sanjari na hayo Mh Katambi amesema swala la madereva kujiunga na vyama vya wafanyakazi ni hiyari ya mfanyakazi sababu sheria ya ajira na mahusiano kazini sura namba 366 inakataza waajiri kuzuia wafanyakazi kujiunga na vyama husika.

Serikali itaendelea kutoa elimu kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji kuhusu umuhimu wa wafanyakazi kujiunga na vyama na kuchukua hatua kwa waajiri watakao zuia kujiunga na vyama hivyo kwasababu ipo kwa mujibu wa sheria” amesema Mh Katambi.

Vilevile amesema Serikali imeondoa baadhi ya Vituo vilivyokuwa vinalalamikiwa kwa sasa magari hayatalazimika kuingia kila kituo badala yake mabasi katika vituo vikuu tu .

LATRA imeshatoa ratiba mpya ya kutekeleza swala hili ,swala la kwamba hapa kituo hapa ushuru lazima uingie kituoni hata kama huna abiria unaemshusha agizo la Serikali ni kwamba mabasi yataenda na kuingia kwenye vituo vukuu tu“amesema Mh Katambi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!