Home Kitaifa SERIKALI ITAENDELEA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

SERIKALI ITAENDELEA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazimgira Dakta Seleman Jafo, imesema itaendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria ya utunzaji wa Mazingira ikiwemo maeneo ya Baharini ili kulinda Viumbe na Mazalia ya Bahari pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Waziri Jafo, ametoa Kauli hiyo mara baada ya kuzindua Kampeni ya Usafi wa Visiwa vya Bahari ya Hindi Kusini mwa Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelelezaji wa zoezi la usimamizi wa Usafi.

Pamoja na mambo mengine Jafo ,amesema Wizara yake haitasita kuwachukulia hatua za Kisheria watu watakao bainika kufanya uharibifu wa mazingira.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Fatuma Nyangasa , pamoja na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo ya Wirara ya Mazingira amesema Ofisi yake inaendelea kuimarisha usalama katika maeneo yaliyopo kwenye Mwambao wa Bahari ili hatimaye ardhi pamoja na mazingira kwa ujumla wake viisiharibiwe

Baadhi ya Mabalozi wa Mazingira kutoka Mikoa Tofauti iliyopo nchini nao kwa nafasi yao wakatoa wito kwa watanzania kuzingatia usimamizi wa mazingira ya bahari.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!