Home Kitaifa RC MALIMA ATOA MASAA 24 KWA WATENDAJI WANAOSIMAMIA HUDUMA ZA KIJAMII, MSOMERA

RC MALIMA ATOA MASAA 24 KWA WATENDAJI WANAOSIMAMIA HUDUMA ZA KIJAMII, MSOMERA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima ametoa saa 24 kwa watendaji wanaosimamia miundombinu ya huduma za kijamii na sekta ya mifugo kwa wananchi wa kijiji cha Msomera wilayani Handeni waliohamia kutoka Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro iwe imekamilika.


Malima ametoa kauli hiyo katika kikao na wananchi hao na watendaji, kusikiliza changamoto zinazowakabili tangu wamehamia kijiji hapo wiki iliyopita, ambapo kati ya changamoto zilizoibuka ni kutambua njia za kupitisha mifugo, mabwawa ya maji kwa ajili ya kunyweshea mifugo , maeneo ya malisho na josho.
 
“Nataka ninapoondoka hapa leo, kesho nikiruidi hapa tuondokane na changamoto hizi. Inawezekana kwenye mfumo wote tulioweka hatujatimiza au hatujafanikiwa kwa yale yote kama tulivyotaka lakini yako mambo ya msingi ambayo tulikubaliana, tulisema mifugo ikija lazima ipate sehemu ya maji,” amesema Malima.
 
“Hakuna kero kuna changamoto, na ukweli ni kwamba watazoea kama sisi tulivyozoea kwa sababu tunajua kabisa wakati tunasubiri kupokea ugeni huu wote tumejitahidi hakuna idara ambayo haijajjitahidi kutimiza wajibu wake,”
 
“Na ndiyo maana nasema mimi nitahamia huku na ikiwezekana katika zile nyumba moja nitachukua mimi nitakaa hapa mpaka kitaelekeweka. Kwa hiyo hayo yote matatu nataka yakamilike leo yaani kesho tuondokana na changamoto hizo,” amesema.
 
“Nataka mambo hayo matatu yawe yamekamilika wageni wangu hawa wawe wamejua maeneo hayo waliyoainisha wajue kabisa kwamba ng’ombe zao zinapita hapa siyo huu mpango wenu wa A, B, C, D… hawauelewi hata miomi siuelewi,” amesema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!