Home Kitaifa TUNAFUATILIA MWENENDO WA UWEPO WA TEMBO KATA YA MKIWA NA MISUGHAA

TUNAFUATILIA MWENENDO WA UWEPO WA TEMBO KATA YA MKIWA NA MISUGHAA

Tumeendelea kupokea na kufuatilia mwenendo wa taarifa za uwepo wa TEMBO katika maeneo ya kata za Mkiwa na Misughaa wilaya ya Ikungi

Ofisi ya mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na mamlaka zingine wanaendelea kuwafuatilia Tembo wanaonekana katika makazi ya watu katika maeneo tajwa

Aidha ofisi ya wilaya kwa kushirikiana na mamlaka zingine imefanya kikao kazi na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith S. Mahenge Jana Tarehe 20/06/2022 na kukubaliana kuchukua hatua zaidi za kudhibiti Tembo walioko kwenye makazi ya wananchi

Kwa Taarifa hii, tunaomba wananchi katika maeneo tajwa kuendelea kuchukua tahadhari ya usalama wao, pia tunaomba wananchi kuacha Tabia ya kuwashambulia, kuwakimbiza au kuwasongasonga Tembo wanaopita katika maeneo yao badala yake watoe taarifa kwa mamlaka husika za vitongoji, vijiji, kata na hata wilaya

Ofisi ya Mkuu wa wilaya Ikungi inapenda kuwahakikisha wananchi Serikali inafanya kila linalowezekana katika mamlaka zetu kuondoa changamoto kwa haraka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!