Home Kitaifa RAIS SAMIA AMEANDIKA HISTORIA UJENZI UWANJA WA MSALATO

RAIS SAMIA AMEANDIKA HISTORIA UJENZI UWANJA WA MSALATO

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema CCM inapongeza kwa dhati Rais Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kwa kuandika historia kwa taifa baada ya miaka kadhaa tangu kuwekwa azimio la makao makuu ya nchi kuhamia mkoani Dodoma.

Shaka ameyasema hayo leo Oktoba 30, 2022 Msalato mkoani Dodoma alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua ni kwa kiasi gani CCM inaridhishwa na utekelezaji wa Ilani yake ya Uchaguzi baada ya Rais Samia kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwnja wa ndege wa Kimataifa wa Msalati mkoani humo.

“Kama tulivyosikia Oktoba mwaka 1973 ndipo lilipotangazwa azimio la kuhamia hapa Dodoma. Tangu mwaka 1973 hadi leo zimepita awamu mbalimbali na kila awamu ilichukua sehumu ya utekelezaji wa uamuzi huo. Katika awamu hii ya sita ya ndugu Samia Suluhu Hassan kasi ya utekelezaji wa uwamuzi huo imekuwa kubwa sana.

Kwenye hili Rais Samia amefanya vizuri sana, tukiangalia uendelezaji mji wa serikali wote tumeona awamu ya tano imefanya vizuri, imetoa karibu sh. bilioni 39 katika uendelezaji wa mji huo, lakini awamu ya sita imechochea na kukoleza, Rais Samia tayari ameshaidhinisha sh. bilioni 300 kwa ajili ya uendelezaji mji wa serikali,” amesema.

Shaka amesema hatua hiyo inaonyesha namna ambavyo maazimio na uamuzi wa Chama Cha Mapinduzi unavyotekelezwa, na kusisitiza kuwa” kwenye hilo niseme tulikotoka ni kuzuri, tulipo ni pazuri zaidi lakini mwelekeo wetu ni kuwa imara zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!