Home Kitaifa RAIS SAMIA AFUNGUA KONGAMANO LA KITAIFA KUHUSU NISHATI SAFI YA KUPIKIA ”TANZANIA...

RAIS SAMIA AFUNGUA KONGAMANO LA KITAIFA KUHUSU NISHATI SAFI YA KUPIKIA ”TANZANIA CLEAN COOKING CONFERENCE” JIJINI DAR ES SALAAM

Na Mercy Maimu

Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kuundwa kwa kikosi kazi cha kushughulikia matumizi ya Nishati safi ya kupikia ili kuondokana na athari za Mazingira na kiafya kwa Watanzania kitakachoongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.


Ametoa maelekezo hayo wakati akifungua Majadiliano ya Kitaifa kuhusu Nishati Safi ya kupikia yaliyoandaliwa na Wizara ya Nishati ambapo amesema timu hiyo Maalum ihusishe Sekta mbalimbali za Serikali na binafsi ili kuangalia sera na Mipango ambapo amesema lengo hadi kufikia 2032 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia Nishati hiyo.


Hii inaonyesha bado kuna kazi ya kuhamasisha matumizi ya nishati iliyo safi na salama. Tunapaswa kuwa na mkakati madhubuti wa kisera na kibajeti pamoja na kuweka mazingira wezeshi katika kutatua changamoto za upatikanaji wa nishati safi“.


“Kwenye hili Serikali peke yetu hatuwezi tunapaswa kwenda sambamba na sekta binafsi, nashukuru baadhi yao wameanza kujitokeza tunakwenda nao sambamba lakini si kisera kwa sababu ni fursa ya biashara hivyo kuna haja ya kuwa na sera inayoshughulikia suala hili,” amesema Rais Samia.


Aidha Rais SAMIA amesema tatizo la Maji linaloikumba hivi Sasa linatokana na ukataji wa miti kwa ajili ya matumizi ya Kuni na mkaa huku akimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Pwani kufuatilia Watu wanaochepusha Maji kutoka Ruvu.
Waziri wa Nishati January Makamba akiongoza mjadala kuhusu Nishati hiyo amesema pamoja na athari za Kimazingira mamilioni ya Watanzania wanaathirika kiafya kutokana na matumizi ya Nishati chafu ya kupikia huku Watoto wengi wakiwa hatarini kukosa Masomo.


Watoto na wanawake wanatumia muda mwingi kutafuta Kuni hali ambayo inawasababishia kusababisha ukatili kwenye ndoa zao na Kwa watoto kupeleka kuacha masomo


Wakizungumza katika Majadiliano hayo Waziri Mstaafu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka, Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Fedha, Shirika la Umoja wa Mataifa na Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) Emmanuel Muro wamesema ili kuondoka kwenye tatizo hilo Nishati mbadala ipatikane kwa bei nafuu.


Watu wanashindwa kuacha kutumia mkaa kutokana na bei ya gesi kupanda,mtungi mdogo wa gesi ulikutwa ni sh 18000 lakini kwa sasa umepanda hadi sh 24000“. Pia EWURA inabidikuweka bei nafuuili kusaidia kaya za hali ya chini kuweza kutumia gesi
Kongamano hilo ambalo ambalo linafanyika kwa siku mbili limehusisha Wadau mbalimbali wanaozalisha Nishati Safi ya kupikia ambapo pia mada mbalimbali kutoka kwa watalaam zinawasilishwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!