Home Kitaifa OFISI ZA TAASISI ZA MUUNGANO KUFUNGULIWA ZANZIBAR KWA HUDUMA BORA

OFISI ZA TAASISI ZA MUUNGANO KUFUNGULIWA ZANZIBAR KWA HUDUMA BORA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amesema usimamizi makini wa utekelezaji wa Mambo ya Muungano umeleta mafanikio katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
 
Amesema yaliyopatikana yaliyopatikana ni kuimarika kwa utaifa na umoja, amani na utulivu na hali ya maisha ya wananchi kutokana na ukuaji wa uchumi wa pande zote mbili za Muungano.

Mhandisi Masauni amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kuanzishwa kwa Akaunti ya pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mchakato wa kuundwa kwa Tume ya kusimamia akaunti hiyo kwenye Kamati ya kudumu ya Bunge ya kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria jijini Dodoma leo Januari 25, 2025.
 
Ameongeza kuwa utekelezaji wa Mambo ya Muungano kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yale yasiyo ya Muungano unakwenda sanjari na mipango, sera, programu na mikakati ya maendeleo ambayo Serikali zote mbili zimejiwekea kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa Watanzania.
 
Ili kuwa na tija katika utekelezaji na kusogeza huduma karibu na wananchi wa pande zote mbili za Muungano, Serikali imehakikisha Taasisi za Muungano zinajenga au kufungua Ofisi Tanzania Bara na Zanzibar. Taasisi hizo zimekuwa zikitekeleza majukumu yake Zanzibar kupitia utaratibu wa mashirikiano na Taasisi za Zanzibar zenye kufanana katika majukumu,” amesema.
 
Aidha, Mhandisi Masauni amesisitiza kuwa Taasisi zote za Muungano zinatakiwa kuwa na Ofisi Zanzibar, hivyo Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kuzielekeza ambazo hazijafungua Ofisi Zanzibar ili kusogeza huduma karibu na wananchi wa Zanzibar.
 
Katika hatua nyingine, amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zinaendelea kushughulikia suala la ufunguaji wa Akaunti ya Fedha ya Pamoja ili kuhakikisha masuala ya mgawanyo wa fedha yanaratibiwa na kusamimiwa kwa ufanisi kwa faida ya pande zote mbili za Muungano.
 
Amesema utaratibu wa kuchangia fedha zitakazowekwa kwenye
Akaunti ya Fedha Pamoja na matumizi ya fedha hizo, umependekezwa na Tume ya Pamoja ya Fedha na kuwasilishwa kwa Serikali mbili kupitia Ripoti ya Mapendekezo ya Vigezo vya Kugawana Mapato na Kuchangia Gharama za Muungano.
 
Katika kufikia uamuzi kuhusu mapendekezo hayo, Waziri Masauni amesema Serikali mbili zinaendelea na mashauriano kuhusu utaratibu wa kudumu wa Kuchangia Matumizi na Kugawana Mapato ya Muungano hivyo, uamuzi wa pamoja utakapofikiwa na pande mbili za Muungano, ndiyo utakaowezesha kufunguliwa kwa Akaunti ya Fedha ya Pamoja.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama amepongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa utekelezaji wa majukumu yake.
 
Mhe. Dkt. Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Madaba amesema Kamati hiyo itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais ili iendelee kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
 
Hivyo, sanjari na uwepo wa Taasisi mbalimbali za kimuungano Zanzibar, pia taasisi za kimuungano zinazotarajiwa kujengwa Zanzibar ni Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na Ofisi ya Taifa ya Takiwmu (NBS).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!